Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA), Bruno Mteta, alisema jana katika mkutano na wanahabari uliofanyika jijini Dar es Salaam.
“Katika kipindi cha kuanzia Septemba mwaka jana hadi Julai 2013, wakala umewakamata wator
oshaji wa madini katika matukio 25 tofauti kwenye viwanja vya ndege vya kimataifa vya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza”, alisema.
Alisisitiza kuwa Jumanne wiki hii katika matukio tofauti, TMAA iliwakamata raia wawili wa kigeni kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam na mwingine alinasawa akiwa na madini nyumbani kwake Jangwani Beach- Dar es Salaam.
Licha ya Mteta kukataa kutaja majina na uraia wa watuhumiwa hao, alisema aliyekamatwa uwanja wa ndege alikuwa na aina mbalimbali za vito yenye thamani ya Dola 15,826 sawa na Sh. milioni 25.32 na kwamba, mbali na kumchukulia hatua za kisheria, madini aliyokamatwa nayo yametaifishwa.
“Huyo raia mwingine alikamatwa na wakaguzi wa TMAA kwa ushirikiano na polisi, usalama wa taifa na ofisi ya madini kanda ya Mashariki akiwa na shehena ya vito nyumbani kwake na kwamba uthamanishaji unaendelea na yanaonekana yana thamani kubwa,” alisema Mteta.
Katika matukio ya ukamataji watorosha madini, alisema raia wa kigeni ni wengi ikilinganishwa na manne yaliyowahusisha Watanzania.
KUDHIBITI UTORASHAJI
Alisema madini yanayotoroshwa ni tanzanite, rubi, safaya, ganeti na tomalini ambayo yanaweza kutoroshwa kwa urahisi kwa kuwa mashine za ukaguzi kwenye viwanja vya ndege haziwezi kugundua madini ambayo si jamii ya chuma kama dhahabu na shaba.
Aliwaambia wanahabari kuwa vito vinaweza kusafirishwa kwa kuwekwa ndani ya mizigo mingine ndani ya mabegi ya wasafiri bila kugundulika ndiyo maana vinatoroshwa kwa urahisi.
“Hata hivyo, mwisho wa wizi huo unakaribia kwani TMAA inawasiliana na wataalamu wa madini wa Kongo ambao wameagiza kutoka Israel x-ray mahsusi za kubaini vito katika viwanja vya ndege na sehemu nyingine za usafiri kama bandarini, mipakani.”
Alisema pamoja na kufikiria uwezekano wa kuagiza mitambo hiyo ya kukagua vito , jitihada zinafanywa kwenye viwanja vya ndege kupekuwa mizigo ya wasafiri.
MADALALI MATAPELI
Mteta alionya kuwa utoroshaji wa madini unaofanywa na wageni unafanikishwa na Watanzania ambao ni madalali ama kampuni zenye leseni za kuuza madini hayo.
Aliongeza kuwa wafanyabiashara hao wasio waaminifu huwauzia madini wageni bila kuwaelekeza kuwa wanatakiwa kulipa kodi za serikali kabla ya usafirishaji huo.
“Wako wasiowaaminifu ambao huwauzia na kuwadai kodi za serikali ambazo baada ya kupatiwa wanazila na wafanyabiashara wanapokamatwa wanaeleza kuwa walilipia lakini wanapokamatwa hakuna uthibitisho.”
KENYA KUZUIA UTOROSHAJI TANZANITE
Aliwaambia wanahabari kuwa katika jitihada za kudhibiti utoroshaji wa tanzanite kupitia Kenya , Tanzania imewasiliana na Kenya juu ya kuanzisha tozo na kodi ya mrahaba ili wanaopitisha wabanwe.
Licha ya tanzanite kupatikana Tanzania pekee hutoroshwa kwa wingi kupitia Kenya ambako wafanyabiashara hawatozwi ushuru wala mrahaba.
Alisema viongozi hao wa madini wamefikia hatua kubwa za majadiliano na wanakusudia kusaini hati ya makubaliano (MOU) kuwezesha utekelezaji wake.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment