KITENDO cha Rais Jakaya
Kikwete kumuita ikulu mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’ kisha kumsaidia
kumtoa kwenye dimbwi la utumiaji wa madawa ya kulevya, kimesababisha kiongozi
huyo wa nchi kulazimika kuwaita na mateja wengine ili kuzungumza nao.
Rehema
Chalamila ‘Ray C’.wenye Kituo cha Pili
Missana Foundation kilichopo Kigamboni jijini Dar, walitinga Ikulu Jumanne
iliyopita huku wakiwa wameong
ozana na mfadhili wa kituo hicho, Zachakia Hans
Poppe pamoja na wadau wengine.Akizungumza na Ijumaa juzi, mmoja wa wakurugenzi wa kituo hicho, Pili Missana alisema wamefarijika sana kupata mualiko huo na wanaamini ni hatua mojawapo kuelekea kwenye kulikabili vilivyo tatizo la matumizi ya ‘unga’ nchini.
Rehema
Chalamila 'Ray C' alipokuwa akimshukuru Rais Kikwete kwa msaada wa matibabu.
(Picha na Ikulu).
Naye Rais JK katika
kukisaidia kituo hicho, ameitaka Wizara ya Afya kupitia Kitengo cha Magonjwa ya
Akili na Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Madawa ya Kulevya kushirikiana nacho ili
kiweze kuwasaidia vijana wengi kadiri inavyowezekana.
na GLOBAL PUBLISHERS
0 comments:
Post a Comment