Binti na mtoto waliofanyiwa unyama.
MTANZANIA mwenye asili ya Kihindi, aitwaye Mohammed
anayetuhumiwa kumlawiti mtoto wake wa kufikia na kumbaka shemeji yake hivi
karibuni, ametoa vitisho vya kumuua mzazi mwenziwe kwa kutoa taarifa ya matukio
hayo polisi, Mohammed ambaye alitoroka Kigamboni jijini Dar
alikokuwa akiishi na mzazi mwenziwe huyo, pia ametishia kuich
oma moto nyumba anayoishi mwanamke huyo ambaye amezaa naye mtoto mmoja.
oma moto nyumba anayoishi mwanamke huyo ambaye amezaa naye mtoto mmoja.
Akizungumza mzazi mwenza wa Mohammed
aliyefahamika kwa jina la Zubeida alisema baada ya mwanaume huyo kubaini
analifuatilia sakata lake la kuwafanyia vibaya watoto hao, amempigia simu na
kumpa vitisho kwamba ajiandae kuvamiwa usiku na kuchomewa nyumba anayoishi.
“Sina amani kabisa na hata hawa polisi siwaelewi kwa
kuwa simu ya mtuhumiwa inapatikana na ananipigia kunitishia lakini wanashindwa
kumkamata, nahisi kuna mchezo unaendelea kwani Mohammed ameniambia nisihangaike
na polisi kwa sababu hakuna anayeweza kumkamata,” alisema mama huyo.
Mama huyo ameendelea kusema kwamba Kituo cha Polisi
Kigamboni hawampi ushirikiano wa kutosha na aliamua kwenda kwa Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Englbelt Kiondo aliyemshauri aende kwa
mpelelezi wa kesi ambaye angemwandikia barua ya kukamatwa kwa mtuhumiwa.
“Jambo hilo nimeliona kuwa ni gumu sana kwangu,
nahitaji msaada na naomba Watanzania wanisaidie kwani sina amani kiukweli,”
alisema.
Aidha, mama huyo ameziomba taasisi zinazoshughulikia
masuala ya haki za binadamu na watoto zimsaidie katika suala hilo kwani hana
njia nyingine ya kuweza kupata msaada.
Kama vile haitoshi, mama huyo ameomba msaada wa
kutibiwa kwa watoto wake kwa kuwa wameathirika kwa kiasi kikubwa.
Mohammed anadaiwa kumlawiti mtoto wa kiume wa mama
huyo mwenye umri wa miaka sita aliyekuwa akilala naye chumba kimoja baada ya
mkewe kujifungua.
Aidha, mdogo wa mkewe alipofika nyumbani hapo,
inadaiwa mtuhumiwa huyo alikuwa akiamka usiku na kujidai kwenda kuvuta sigara
kumbe alikuwa akienda kumbaka.
Gpl
0 comments:
Post a Comment