BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ROBEERT MUGABE AVUNJA REKODI NAAPISHWA KUIONGOZA ZIMBABWE KWA AWAMU YA SABA.

Robert Mugabe anaapiswa leo kuwa rais wa Zimbabwe kwa awamu ya saba mfululizo.

Siku hii ya leo ya Alhamisi imrtangazwa kuwa siku ya mapumziko nchini humo ili kuwapa nafasi wafuasi wanaomuunga mkono rais huyo mwenye miaka 89 kuhudhuria sherehe za kuapishwa zinazofanyika katika uwanja mkubwa wa michezo mjini Harare.

Sherehe hizo za kuapishwa zilikuwa zikicheleweshwa na pingamizi mahakamani lilifunguliwa na mpinzani wake mkubwa Morgan Tsvangirai kwa madai ya kuwa uchaguzi uligubikwa na udanganyifu.

Hata hivyo mahakama ya katiba ilitumbilia mbali kesi hiyo, na kutangaza kuwa kuchaguliwa kwa Mugabe kulikuwa kwa huru na kwa haki.

 Mugabe alipata asilimia 61 ya kura za urais dhidi ya asilimi 34 za Tsvangira katika uchaguzi wa Julai 31 mwaka huu.

Uchaguzi huo umemaliza serikali ya kugawana madaraka iliyoundwa na viongozi hao wawili mwaka 2009, chini ya shinikizo la viongozi wa Ukanda wa Afrika, kufuatia uchaguzi uliokuwa umefanyika mwaka mmoja kabla kugubikwa na vurugu na madai ya wizi wa kura.

Waziri Mkuu wa zamani na Kiongozi wa Upinzani Tsvangira amesema hatahudhuria sherehe hizo za kuapishwa.

Wakato huo huo Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete na ujumbe wake wako mjini Harare kuhudhuria sherehe hizo zinazofuatia ushindi wa Rais Mugabe na chama chake cha ZANU-PF katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini humo Julai 31, mwaka huu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: