Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hellen Riwa.
Wakili wa serikali Leonard Challo alidai kuwa Agosti 4, mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere alikamatwa na askari akiingiza kilo 1,512.69 za dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride zenye thamani ya Sh. 68,069,250.
Katika shtaka la pili ilidaiwa kuwa siku na tarehe ya tukio la kwanza mshtakiwa alikamatwa na askari akiingiza nchini dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gramu 34.77 yenye thamani ya Sh.13, 908,000.
Wakili Challo alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Hata hivyo, Hakimu Riwa alisema mshitakiwa hatakiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi ya dawa zenye thamani zaidi ya Sh. milioni 10.
Aidha, kesi hiyo upelelezi wake utakapokamilika itasikilizwa Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Mshitakiwa alikana shtaka la pili la kukamatwa akiingiza bangi nchini.
Hakimu Riwa alisema mshitakiwa apelekwe mahabusu hadi Septemba 3, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa. SOURCE: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment