WAKATI
viongozi wa Kanisa la Orthodox jijini Dar es Salaam wakidai kuwa
hawataki Klabu ya British Legion of Tanganyika kuendesha shughuli zao
katika eneo wanalodai ni lao kwa madai ya kuwepo kwa picha chafu na
ulevi, sakata hilo limeibua mapya baada ya maaskofu kudai kuwa
wamekashifiwa.
Maaskofu
wa kanisa hilo, wamedai kukashifiwa na kudhalilishwa na Mwenyekiti wa
Klabu, Abdul Mtiro Sisco kutokana na kiongozi huyo kuwaambia waandishi
wa habari kuwa eneo la klabu yao linataka kuuzwa na kanisa kutokana na
dhiki waliyonayo Wagiriki.
Mtiro
alidai kwa waandishi wa habari kuwa kutokana na matatizo ya kiuchumi
nchini kwao, Wagiriki hao wanataka kuliuza eneo hilo ili wapeleke fedha
kwao.

Mwenyekiti wa Klabu, Abdul Mtiro Sisco.
“Wanadai
kuwa hapa sisi tun
afanya uhuni wakati watu wanaokuja hapa si wahuni…Hawa Wagiriki kwa sababu ya matatizo ya uchumi nchini kwao, wanataka kuuza eneo hili ili wawapelekee fedha ndugu zao…” alidai Mtiro.
afanya uhuni wakati watu wanaokuja hapa si wahuni…Hawa Wagiriki kwa sababu ya matatizo ya uchumi nchini kwao, wanataka kuuza eneo hili ili wawapelekee fedha ndugu zao…” alidai Mtiro.
Mtiro
alidai klabu yao ipo hapo tangu mwaka 1970 kama British Legion of
Tanganyika ambapo awali ilikuwa ni ya wanajeshi wa Uingereza lakini
baadaye Waafrika wakaingia lakini ugomvi wao ulianza mwaka 1990
walipoambiwa watoke eneo hilo.
Kuhusu madai ya kuwepo picha za utupu ndani ya klabu hiyo, Mtiro
alisema si kweli, hata hivyo, akasema kwamba hiyo ni klabu binafsi.
Habari zinasema kauli hiyo imewaudhi maaskofu wa kanisa hilo na
kuwafanya kuwasiliana na wanasheria wao ili kuona jinsi ya kushughulikia
hicho wanachodai kuwa ni kashfa kwao.

Baadhi ya viongozi wa kanisa.
Askofu
mmoja wa kanisa hilo amesema hawakubaliani na madai ya Mtiro kwa sababu
ndani ya klabu hiyo kulikuwa na picha za utupu na wanafanya biashara ya
pombe eneo la kanisa.“Lengo letu sisi ni kuwafundisha watu wamfuate
Mungu waende Mbinguni na tunaomba maeneo yote ya kanisa yaheshimiwe,”
alisema askofu mmoja.
Wakati
hayo yakiendelea, sakata la kugombea eneo hilo tayari limefikishwa
Mahakama Kuu chini ya Jaji John Mgetta ambapo upande wa kanisa, Wakili
Edward Chuwa amedai kuwa wamezuia kuingia wanachama wa klabu hiyo kwa
sababu hawawajui na hakuna mahali panapoonesha wanachama ni akina nani.
Upande wa klabu ukiongozwa na Wakili Evod Mmanda katika kesi hiyo
namba 178/2013, wamedai mbele ya jaji huyo kuwa kanisa lisiwepo katika
eneo hilo na wanachama waruhusiwe kuingia katika klabu yao wakati shauri
likiendelea kusikilizwa mpaka hapo mahakama itakapotoa uamuzi.
Jaji Mgetta alitembelea eneo hilo Jumanne iliyopita na kesi hiyo
itaendelea kusikilizwa Agosti 21, mwaka huu ambapo mahakama itasikiliza
pingamizi lililowekwa na kanisa
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari

0 comments:
Post a Comment