
NCHINI Uingereza Gazeti la Daily Mail linalotoka
kila siku limeandika kwamba, Katibu wa Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Shehe Issa
Ponda Issa anaweza kuwa mtuhumiwa mkuu wa tukio la wasichana wawili raia wa
nchi hiyo waliomwagiwa tindik
ali hivi karibuni.
Kirstie Trup (18) na Katie Gee (18t), wakazi wa
Hampstead, Kaskazini-Magharibi mwa London ambao wanatibiwa hospitali moja
nchini humo, walimwagiwa tindikali Agosti 7, mwaka huu huko visiwani Zanzibar,
madai makubwa yakiwa ni kuvaa mavazi yasiyoendana na Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani.
MAHUBIRI YA PONDA YATAJWA
Pamoja na kupigwa risasi begani huko Morogoro, kwa
mujibu wa gazeti hilo lililoingia mtaani Jumatatu iliyopita, pamoja na kutomhusisha
moja kwa moja, Shehe Ponda aliwahi kutoa mahubiri Zanzibar ambayo kwa akili ya
kawaida ni kama yalichochea wasichana hao kumwagiwa tindikali.
Gazeti hilo liliandika kuwa kuna uwezekano Kikundi
cha Uamsho kuhusika huku mahubiri ya Ponda yakihusishwa na utendaji wa kundi
hilo, jambo ambalo hata polisi wanalihisi.
Gazeti hilo lilidai kuwa Shehe Ponda alipigwa risasi
huko Morogoro huku akiwa anasakwa huko Zanzibar kwa sababu ya mahubiri
yaliyosemekana yalikuwa ya kichochezi.
“Alitembelea Zanzibar wiki kadhaa zilizopita na
baada ya mahubiri ya chuki aliyoyatoa kwa wafuasi wake akiwataka kuandamana
kupinga ukoloni ndipo Kirstie na Katie wakamwagiwa tindikali.
“Tindikali imekuwa ndiyo silaha kubwa Zanzibar
ikitumiwa na kundi hilo linalotaka kujitenga katika nchi ya Tanzania na
kuongozwa na Sharia,” liliandika Dail Mail la Uingereza.
GAZETI LINGINE
Gazeti lingine la The Telegraphic la nchini humo
liliandika: “Shehe Ponda alitumia wiki nzima Zanzibar mwanzoni mwa Agosti
akihubiri misikitini akiunga mkono maandamano ‘kama ya Misri’ hadi ‘memba’ wao
10 waliofungwa waachiwe.
“Alikuwa akizunguka akiwaambia vijana wafanye
maandamano yasiyokuwa na kikomo kuonesha wao wana nguvu.”
MTANZANIA AISHIYE LONDON AFUNGUKIA HALI ILIVYO
Mtanzania aishiye Jiji la London, Uingereza (jina
tunalo) aliliambia Risasi Mchanganyiko juzi kwamba, baadhi ya Waingereza
wametokea kumchukia Shehe Ponda baada ya habari yake na picha kuchapishwa
kwenye gazeti hilo likimhusisha na tindikali ya wasichana hao waliokuwa
wakijitolea kufundisha huko Zanzibar.
“Waingereza wengi wametokea kumchukia Shehe Ponda
huo ndiyo ukweli. Wanasema kama Tanzania hawataichukulia ‘siriasi’ ishu hiyo,
basi Shehe Ponda siku akitua London, itakula kwake,” alisema Mbongo huyo.
Aliongeza kuwa sera ya Uingereza tangu Mkutano wa
Berlin, Ujerumani mwaka 1884/85 wa nchi za Ulaya kuweka maazimio ya kuitawala
Afrika, kila nchi ilitakiwa kulinda watu wake hivyo sera ya Uingereza kwa sasa
ni kulinda raia wake wa nje na ndani kwa gharama zozote zile.
“Unakumbuka ule Mkutano wa Berlin mwaka elfu moja
mia nane na themanini na nne, nchi za Ulaya ziliweka maazimio kuhusu kujilinda
na kuingia katika makoloni ya Afrika.
“Uingereza iliamua kuweka sera ya kulinda raia wake
wa ndani na nje kwa gharama yoyote ile.
“Ndiyo maana naweza kusema Ponda atachukiwa tu mpaka
mwisho. Unajua Waingereza siku zote wanawachukia watu wenye misamamo mikali,
watu wanaoweza kufanya lolote bila kujali uhai wa mtu mwingine,” alisema
Mtanzania huyo.
WABONGO WAITAKA SERIKALI KUMWONGEZEA ULINZI PONDA
Jijini Dar es Salaam, juzi baadhi ya watu
waliozungumza na gazeti hili nje ya wadi aliyolazwa Shehe Ponda, Hospitali ya
Muhimbili waliitaka serikali kumwongezea ulinzi kiongozi huyo.
Bakari, mkazi wa Kigogo, Dar alisema: “Tayari
magazeti ya Ulaya yameanza kumtuhumu Ponda kwamba alichochea wale Wazungu
kumwagiwa tindikali, ni vyema kama serikali ikawa makini naye.
“Wenzetu (Waingereza) wana uwezo mkubwa na zana
kibao, wanaweza kutua juu ya paa la hospitali hapa wakamchukua na kumpeleka
Uingereza.”
KISA CHA PONDA NA SERIKALI
Licha ya watu kuitaka serikali kumlinda zaidi Shehe
Ponda, tayari kiongozi huyo yuko chini ya ulinzi hospitalini alikolazwa.
Inadaiwa kuwa Shehe Ponda akipona atafikishwa mbele
ya sheria kujibu tuhuma za uchochezi wakati akihubiri huko Zanzibar hivi
karibuni wakati bado akiwa kwenye kifungo cha nje baada ya kuhukumiwa kifungo
cha nje miezi kadhaa iliyopita.
Wakati hayo yakiendelea Bongo, huko London wasichana
waliomwagiwa tindikali wanaendelea na matibabu katika Hospitali za Chelsea na
Westminster ikielezwa kuwa mmoja atawekewa ngozi ya bandia kutokana na
kuharibiwa kupita maelezo.
Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete alilaani vikali kitendo cha kinyama walichofanyiwa
wasichana hao kwa maelezo kuwa ni aibu kwa Tanzania

0 comments:
Post a Comment