VIGOGO 111 wanaosadikiwa
kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya nchini wameanza
kuonja 'joto ya jiwe' kufuatia Jeshi la Polisi Tanzania Kitengo cha
Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya kwa kushirikiana na vyombo
vingine vya dola kukamata mali zao.
Kwa mujibu wa vyanzo makini
ndani ya jeshi hilo, pia vigogo wengi wanaojihusisha na biashara hiyo
walikam
atwa na kiasi kikubwa cha ‘unga’ ndani ya kipindi cha miaka minne
iliyopita.
Kuhusu mali ambazo ni magari, ilidaiwa kuwa kufuatia
taarifa zilizowataja wauza unga, jeshi la polisi liliamua kushikilia
magari hayo na kufanya uchunguzi wa uhalali wake.
“Kuna watu
walitajwa majina, wakafuatiliwa, magari yao yakakamatwa na kufanyiwa
uchunguzi, lakini cha kushangaza baadhi yao wameingia mitini na
kutelekeza magari yao,” kilisema chanzo.
Chanzo kilisema baadhi
ya magari hayo ni Mercedes Benz, Jeep, Toyota Spacio, Toyota Galsira,
Toyota Mark II, Nissan Patrol 4x4 GL, Toyota Land Cruiser na Toyota
Prado.
Gazeti hili lilifanikiwa kunasa majina ya vigogo waliokamatwa wakiwa na unga na kiasi walichokamatwa nacho.
Uchunguzi
uliofanywa katika mahakama mbalimbali nchini na ndani ya jeshi la
polisi umebaini kuwa, kesi za watuhumiwa hao zinaendelea kuunguruma
kortini japokuwa kasi yake si ya kuridhisha.
Vyanzo hivyo
viliendelea kudai kwamba polisi wamebuni mbinu mpya ya kuwakamata vigogo
wa madawa ya kulevya wakiamini itawapa mafanikio zaidi.
“Siku
hizi si kama zamani, jeshi la polisi tumebuni mbinu mpya ya kuwakamata
hawa jamaa (vigogo). Mbinu hii italeta mafanikio makubwa zaidi,” alisema
mtoa habari wetu.
Taarifa zaidi zinadai kwamba usalama wa
viongozi wanaopambana na wahusika wa unga nchini upo shakani kutokana na
vitisho vinavyotolewa na mtandao huo duniani kote.
Inaaminika
kuwa wengi wanaopambana au kupiga vita madawa ya kulevya, hususan
viongozi na waandishi wa habari, hutendwa vibaya wakati mwingine kuuawa
kabisa.
Kufuatia taarifa hizo za kiuchunguzi, katikati ya wiki
iliyopita, mapaparazi wetu walimtafuta Kamanda wa Kudhibiti na Kupambana
na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa na kumuuliza kuhusu zoezi
zima la kamatakamata ya wanamtandao hao.
Kamanda Nzowa alisema zoezi la kuwakamata wanaojihusisha na biashara hiyo linaendelea vizuri.
Alisema
mpaka Mei, mwaka huu kikosi chake kimeshakamata kiasi kikubwa cha unga
na kuongeza kuwa anaamini kasi ya biashara hiyo nchini imepungua sana.
Aliongeza kuwa askari wake wamejipanga vizuri na wana mafunzo maalum ya kuwatambua watu hao hatari.
“Tumewakamata ‘mapapa’ (wauza unga wadogo) wengi sana na tunahakikisha kwamba ‘nyangumi’ (wauza unga vigogo) nao hawachomoki.
“Mara
nyingi vigogo wamekuwa wakiwalisha kiapo kibaya vijana wanaowabebesha
unga kwamba ikitokea wakakamatwa wasiwataje lakini nao tunawabana
kitaalam mpaka wanawataja, kwa sasa bado tunaendelea kuwadaka,” alisema
Kamanda Nzowa.
Kamanda huyo aliwataka wananchi kuendelea kutoa
ushirikiano kwa jeshi lake dhidi ya wauza madawa ili kutokomeza kabisa
biashara hiyo.
Katika maongezi yake, Afande Nzowa alisema ulinzi
umeimarishwa katika viwanja vya ndege, bandarini, mipaka ya nchi na
sehemu zote zinazohisiwa kuweza kupitishwa madawa hayo.
Kamanda Nzowa alikwenda mbele zaidi kwa kuweka wazi takwimu ya ukamataji wa watuhumiwa hao kutoka mwaka 2009 hadi Mei, 2013.
Orodha chini inabainisha kiasi na aina ya madawa waliyokamatwa nayo katika mabano.
Steven
Gwaza, (heroin gramu 825.7), Rebecca Wairimu Mwangi (heroin gram
1,800), Khatibu Bakari Khatibu, Khalid Salim Maunga, (cocaine gramu
1,007.4), Dhoulkefly Awadh, (cocaine gramu 893.58), Abdallah Pashua
Kipevu (heroin gramu 31,000), Diaka Brama Kaba (heroin gramu 31,000),
huyu alikamatwa akiwa na Ndjane Abubakar, Sylivia Kaaya Namirembe, Farid
Kisuule, Robinson Dumba Teise na Ismail Mugabi.
Wengine ni
Rashid Salim Mohamed, (cocaine gramu 1,374.32), Mini Thabo Hamza
(cocaine gramu 1,595.74), Hamis Mohamed Mtou (cocaine gramu 850), Kwako
Sarfo, Mnigeria (cocaine gramu 1,1951.80), Mustapha Musa (cocaine gramu
286), alikuwa na Aman Saidfadhil Daruweshi na Afshin Jalal.
Kamanda
Nzowa akaendelea kuwaanika, Jack Vuyo, (heroin gramu 42,000) huyu
alikuwa na Anastazia Elizabeth Cloete. Simon Eugenio Fadu (cocaine gramu
8,000), Assad Aziz, (heroin gramu 50,000), alikuwa na Isamil Shebe
Ismail, Rashid Salim na Majed Gholamghader.
Wengine kwenye orodha
hiyo ni, Anna Jamaniste Mboya, (cocaine gramu 1,140), Fredy William
Chonde (heroin gramu 175,000), Kambi Zuber, Abdul Ghan na Shahbaz Malik,
Livinus Malik (Wapakistani) (cocaine gramu 804.7), Chukwudu Denis
Okechukwu, Paulo Ekechukwu na Hycenth Stan (Wanigeria) (cocaine gramu
81,000).
Aidha wapo, Shoaib S.O. Mohammed, Fedro Alfredo Chongo,
(cocaine gramu 1,530), Kadiria Said Kimaro (heroin gramu 1,365.91),
Abdallah Rajab Mwalimu (cocaine gramu 716.5), Mwiteka Godfrey Mwandemele
(cocaine gramu 1,112), Abbas Kondo Gede (cocaine gramu 1,112), Mwanaidi
Ramadhan Mfundo (cocaiane gramu 5,000), alikuwa na Sarah David Munuo,
Antony Karanja, Benny Ngare, Almasi Hamis Said, Yahya Haroun Ibrahim,
Aisha Said Kungwi, Rajab Juma Mzome na John William Mwakalasya.
Wengine
ni Ally Mirzai Pirbakhshi (cocaine gramu 97,000) alikuwa na Aziz Juma
Kizingiti, Said Mashaka Mrisho, Abdulahman Mtumwa na Hamidu Kitwana
Karimu.
Ramadhan Athuman (heroin gramu 3,000) alikuwa na Rashid
Mohammed, Ally Mohammed Kichaa na Issa Abdulahman. Rashid Ally Mtopea
(heroin gramu 12,000) alikuwa na Idd Adam Mwaduga, Nurdin Adam. Maurine
Amatus Lyumba, John Adams Igwenma wa (Mnaijeria) ( cocaine gramu
830.19).
Upendo Mohammed Cheusi, Abdallah Omar Salum (cannabis
sativa gramu 1,000) alikuwa na Cosmos Chukwumezie, Ifeanyi Malven Kalu
Oko (Wanaijeria) (heroin gramu 3,185.38), Allan Duller (cocaine gramu
3,882.92), Alberto Mendes kutoka Ghana, (gramu 1,277.10 za heroin)
Wengine
ni Joseph Chukwumeka Nwabunwanne Minigeria, (gramu 1,245.96 za heroin)
Kwaku Safo Brobbey Mghana (gramu 13,781.78 za heroin), Princewill Ejike
Mnigeria (gramu 981.12 za heroin),Mary Mvula Mzambia (gramu 391.51 za
cocaine), Waziri Shaban Mizongi, (gramu 2,013 za heroin) akiwa na Santos
Joseph Mpondela, Kelvin Kelven Mwazeni.
Wengine ni Emmanuela
Adom, Mghana (gramu 9,838.1 za cocaine), Asha Omary Ramadhan, (gramu
1.56), Mariam Mohammed Said, (gramu 9,857.54 za bangi) akiwa na
Abdullatif A. Fundikira
Aliendelea kuwataja Marceline Koivogui,
Mghana (gramu 1,073.82 za heroin), Edwin Cheleh Swen Mliberia (gramu
1,509.35 za heroin), akiwa na Benjamin Obioma Onuorah wa Nigeria, Sofia
Seif Kingazi, (gramu 3,379.54 za cocaine), Josephine Mumbi Waithera
Mkenya (gramu 3,249.82 za cocaine), Iddi Juma Mfaume,( gramu 563.25 za
heroine), Amina Kassim Ramadhani,( gramu 1,980.11 za heroine) na Vivian
Edigin Mnigeria ( gramu 797.56 za cocaine), Hadija Tambwe,( gramu
33,507.04 Za cannabis), Sasha Farhan na Mnyeke Sativa, na Mychel
Andriand Takahindangeng Muindonesia,( gramu 3,932.44 za cocaine).
Wengine
ni Kristina Biskavevskaja Mluthenia (gramu 4,000 za cocaine), Stephen
Basil Ojiofor Mnigeri (gramu 1,173 za cocaine), Judith Marko Kusekwa, (
gramu 1,793 za heroin), Khamis Said Bakari,( gramu 1,793 za heroin).
Kundi
la mwisho ni Tabia Omary au Neema Omary (gramu 994.97 za heroin),
Masesa au Habiba Andrew Joseph, ( gramu 1,037.9 za heroin).
Hivi karibuni Agness Gerald ‘Masogange’ na mwenzake walikamatwa Afrika Kusini wakiwa na kilo 150 za dawa za kulevya.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / VIGOGO 111 WANAODAIWA KUJIHUSISHA KUSAFIRISHA NA UINGIZAJI WA MADAWA YA KULEVYA WAANZA KUONJA JOTO YA JIWE KUFUATIA BAADHI YA MALI ZAO KUKAMATWA.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment