Jeshi
la Polisi mkoani Arusha limewatia nguvuni watu wanne wanaosadikiwa
kuwa ni majambazi waliohusika katika tukio la tarehe 23 August majira
ya saa nane na nusu mtaa wa Pangani Mjini Kati Arusha,la kuwajeruhi
wafanyabiashara wawili wa madini na kupora kiasi cha shilingi Mil.5 na
madini yenye hamani ya shilingi Milioni 40.
Akizungumza
na vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoa wa Arusha liberatus Sabas
alisema kuwa jeshi la polisi limewakamata watu hao mara baada ya
opareshi ya siku mbili iliyofanywa na Jeshi hilo.
Aidha
kamanda Sabas aalisema kuwa majambazi hayo yamekamatwa na bastola mbili
aina ya Browing Model 83 CAL .9 no 4738 yenye risasi kumi na bastola
ya LAMI yenye risasi 12,gari aina ya Vist yenye namba T368 AUH,Pikipiki
aina ya Skygo,namba T352CBW,na Pikipiki nyiongine aina ya Honda yenye T
464 APH.
Sabas
amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Shangai Willium
Semboni(38)mkazi wa Sokone one,Alli Habibu Hussein au Dogoo au
Sadock(23)mkazi wa Tabata Dar es Saalam,Eugine Donas Mushi maarufu kama
Mbuna(28)mkazi wa makao mapya pamoja na Jerome Shirima (29) mkazi wa
Sombetini.
Alisema
kuwa Wafanyabiashara hao waliojeruhiwa ni pamoja na Aber Musa(35) na
Stephen Aloyce(36) wote wakazi wa Sakina jijini Arusha ambao
walijeruhiwa na wanaendelea kupatiw matibabu.
Kamanda
sabas alisema kuwa majambazi hao wamekiri kuhusika kwenye matukio
mengine ya uhalifu likiwemo kuuwawa kwa mfanyakazi wa kampuni ya Panone
ambaye alipigwa risasi.
Kamanda
Sabas alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi
hilo kwa kuendelea kuwafichua wahalifu ambao wamekuwa wakifanya matukio
mbalimbali ya uhalifu jijini hapa.
Jeshi
la Polisi bado linaendelea kusaka watuhumiwa wengine wawili ili
kuutokomeza kabisa mtandao huo ambapo watuhumiwa hao wametajwa na wenzao
ambao wamekamatwa.
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment