Mwamuzi chipukizi Fikiri Magari (19) moja ya michezo ya waamuzi wa Morosp akiwajibika.
Na Juma Mtanda, Morogoro.
JUMLA ya waamuzi chipukizi nane wa
mchezo wa soka kutoka taasisi ya kuibua na kukuza vipaji vya waamuzi Morogoro
(MOROSP) wanatarajia kuanza kuchezesha michezo ya ligi daraja la tatu na nne
ngazi ya TTF taifa Manispaa ya Morogoro baada ya kuony
esha uwezo mkubwa katika
kuchezesha michezo mbalimbali ya soka mkoani hapa.
Akizungumza na gazeti hili mjini hapa
Mkurufunzi Morosp, Marthin Saanya alisema kuwa taasisi hiyo ina waamuzi
chipukizi zaidi ya 30 wa mchezo wa soka ambao baadhi ya waamuzi hao wanatarajia
kuchezesha michezo ya soka ligi daraja la tatu na nne Manispaa ya Morogoro
msimu wa mwaka 2013/2014.
Saanya alisema kuwa baadhi ya waamuzi
hao nane wameonyesha uwezo mkubwa katika ligi ndogo ndogo zilizopata baraka na
chama cha soka wilaya ya Morogoro (MRFA) ikiwemo mitihani yao ya darasani na
vitendo huku wengi wao wana uwezo wa kuchezesha ligi daraja la tatu hadi nne
TTF taifa ngazi ya mkoa.
Kati ya waamuzi hao ni pamoja na Raphael
Ikamba (18) Juma Shabaan (18) Fikiri Magari (19) Elly Shao (23) Raphael Elisha
(18) Eick Joseph (15) Shabaan Juma (21) na Feruz Ally (13).
“Taasisi hii ina wakufunzi wawili
nikiwemo mimi mwenyewe na Jesse Erasmo na tumegawana kazi ya kuwafunza mimi
nawafunza mambo yote ya uwanjani na mwenzangu yeye mambo ya darasani na sifa ya
waamuzi hawa chipukizi wanacheza sehemu zote mwamuzi wa kati na pembeni”
alisema Saanya.
Saanya alisema kuwa kwa sasa kazi kubwa
iliyopo kwa waamuzi hao ni kuwapa kuchezesha michezo mbalimbali ya ligi
zinazofanyika za kugombea zawadi zikiwemo jezi, mipira, fedha, na wanyama kama
mbuzi na ng’ombe ili kuwapa uzoefu kabla ya kuwachuja na kuingia katika ligi
zenye ushindani.
0 comments:
Post a Comment