MAKULI
zaidi ya 400 wa bandari ya Mwanza wamegoma kupakia na kupakua shehena
ya mizigo kutoka ndani ya meli ya Mv. Victoria na meli zingine
zinazotoka nje ya nchi zinazoegeshwa katika bandari ya mwanza kusini
baada ya uongozi wa mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania (TPA)
Mwanza kusit
isha zabuni ya ubebaji wa mizigo unaofanywa na makuli hao
katika bandari zake.
Mgomo
huo ambao umeanza leo asubuhi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa
wafanyabiashara wanaotumia bandari hizo mbili,umetokana na hatua ya
uongozi wa mamlaka ya bandari Tanzania(TPA) - Mwanza kusitisha mkataba
wa zabuni ya upakiaji na upakuaji wa mizigo katika meli zinazomilikiwa
na mamlaka hiyo, kwa barua iliyosainiwa na Bw. Ngowi kwa niaba ya mkuu
wa bandari ya Mwanza yaagosti 19 mwaka huu.
Makuli
hao ambao pia ni wana ushirika wakiongozwa na mwenyekiti wa ushirika wa
wahudumu wa bandari ya mwanza kaskazini na kusini Rajab Said,
wamepinga kitendo cha kucheleweshwa kutangazwa kwa zabuni na kisha
kupewa nyongeza ya mwezi mmoja kuendelea na shughuli za upakiaji na
upakuaji kwa bandari zote mbili, na wakati huo huo Mamlaka ya usimamizi
wa bandari Tanzania kutangaza zabuni nyingine mpya ni kitendo
kinachoashiria kuwanyanyasa wanaushirika hao na hivyo wamemuomba waziri
wa uchukuzi Mh. Dk.Harrison Mwakyembe kuingilia kati suala hilo ili
kuwabaini baadhi ya viongozi wanaotaka kujinufaisha na zabuni hizo.
Itv
imeshuhudia baadhi ya wafanyabiashara wakiwa katika pilikapilika za
upakuaji wa mizigo yao, ikiwemo mikungu ya ndizi na magunia ya
maparachichi iliyowasili leo asubuhi kwa meli ya Mv. Victoria ikitokea
Bukoba kupitia bandari ya Kemondo baada ya makuli ambao wamekuwa
wakifanya kazi hiyo siku zote kugoma kuingia kazini, huku baadhi yao
wakilalamikia kitendo hicho kwamba kimewasababishiausumbufu mkubwa
ikiwemo kuharibika kwa matunda yao ya ndizi mbivu.
0 comments:
Post a Comment