Na Mwandishi
Wetu
WIKI iliyopita, sexy lady wa Bongo Fleva,
Rehema Chalamila ‘Ray C’ au ‘Kiuno Bila Mfupa’ alifunguka juu ya mwanaume
aliyekuwa akimvutisha madawa ya kulevya ‘unga’ bila kumtaja hivyo kuibua mzozo
katika majukwaa ya kisheria kuwa mtu huyo akamatwe mara moja.
Mara baada ya Ray C kufunguka kuhusu ishu hiyo
kupitia Clouds TV, habari hiyo iligeuka gumzo hasa kwenye mitandao ya kijamii
ikisemekana kuwa mhusika anafahamika.
Ray C alisema mwanaume aliyekuwa akim
uwekea unga bila yeye kujua alikuwa ni boyfriend wake ambaye alitengana naye mwaka 2010 ili kujinusuru na balaa hilo.
uwekea unga bila yeye kujua alikuwa ni boyfriend wake ambaye alitengana naye mwaka 2010 ili kujinusuru na balaa hilo.
Alisema: “Nilimpenda kwa moyo wangu wote ila
nikalazimika kuachana naye.
“Ilibidi aende kwa sababu yeye ndiye
aliyeniletea balaa lote. Nikasema vyovyote vile Mungu naomba unisaidie,
nampenda huyu kijana ila hayupo sawa. Tukatengana 2010 lakini tatizo lilikuwa
limeshaota mizizi.”NA gpl
Kwa mujibu wa baadhi ya wanasheria
waliozungumza na gazeti hili, katika maelezo ya Ray C, mhusika ana kesi mbili
za kujibu, kwanza kuwa na huo unga na pili kumuwekea mtu madawa ya kulevya bila
kujua au hata angejua, yote ni makosa ya jinai.
“Ukiangalia watu kama Rais Jakaya Kikwete na
Ruge Mutahaba walivyojitahidi kumwokoa Ray C utagundua ni jinsi gani
walivyohangaika wakati aliyesababisha yupo !
“Kinachotakiwa kufanyika ni Ray C kumtaja
mhusika ‘theni’ sheria ifuate mkondo wake.
“Ni vema ishu hii ya Ray C ikatumika kama
fundisho kwa mastaa wengine na jamii nzima hasa linapokuja suala la aina ya
mpenzi unayekuwa naye,” aliandika mmoja wa wachangia mada mtandaoni.
Historia inaonesha kuwa mwanadada huyo ambaye
anarejea upya katika muziki aliwahi kuwa na wanaume wawili waliofahamika kila
kona Bongo.
Mmoja ni staa wa Big Brother Africa, Mwisho
Mwampamba ambaye alikuwa mara tu baada ya kutoka kwenye shindano hilo mwaka
2003 ambaye Ray C aliwahi kukiri kuwa walidumu hadi mwaka 2006.
Mwingine ni aliyekuwa rapa wa N2N Soldiers kwa
sasa yuko kwenye Kruu ya Weusi, Waziri Makuto ‘Lord Eyez’ waliyehitilafiana
mwaka 2008

0 comments:
Post a Comment