
TAKRIBANI watu 37 wamekufa baada ya kugongwa na treni wakati wakivuka njia ya reli katika jimbo la Bihar, India. Maafisa wamesema wengi wa abiria walikua mahujaji wa Ki-Hindi waliokua wametua katika kituo kimoja cha eneo la Dhamara Ghat na walikua njiani kuelekea Hekalu iliyoko Wilaya ya Saharsa.
Ajali
hiyo ilipelekea ghathabu ya raia ambao waliteketeza mabehewa ya treni
hiyo. Makundi ya wokozi yanaendelea kutafuta manusura na polisi wa
kuzima ghasia wamet
umwa eneo la ajali.
Mkuu wa
pilisi katika jimbo la Bihar amesema haijathibitishwa idadi kamili ya
watu waliokufa, kwani vipande vipande vya miili ya watu imetapakaa eneo
hilo.
Maafisa
wa huduma ya reli wamesema treni hiyo ya mwendo wa kasi ilikikuwa njiani
na haikutarajiwa kutua kituo cha Dhamara Ghat. Hata hivyo ilisimama
baada ya ajali kutokea ambapo umati wa watu ulishambulia dereva na
kumjeruhi vibaya.
Huduma ya
treni inamilikiwa na serikali nchini India na inawahudumia abiria
milioni 18 kila siku.
Serikali imesema zaidi ya watu laki moja unusu
waliuawa na treni mwaka jana pekee wakati wakivuka njia ya reli
inayotumika na treni za mwendo wa kasi:chanzo bbc

0 comments:
Post a Comment