Nje
ya bunge akilitolea ufafanuzi suala hilo naibu waziri wa uchukuzi Mh
Charles Tizeba amesema suala hilo kwa mara ya kwanza liliibuka katika
mk
utano wa nchi za Afrika ya Mashariki uliofanyika nchini Rwanda ambapo
nchi hizo zilikubaliana kutoza tozo zinazofanana na kwamba mchakato huo
unaendelea.
Kuhusiana
na kuongezeka kwa tozo hiyo naibu waziri huyo amesema baada ya kupata
taarifa hizo kwa haraka amewasiliana na waziri wa miundo mbinu wa
Rwanda aliyemtaja kwa jina la Prof Rwakabamba ambaye amekiri uwepo wa
hatua hiyo ya kupandisha tozo hiyo kutoka dola za kimarekani 152 hadi
kufikia dola za kimarekani 500 kwa magari yaliyosajailiwa Tanzania na
kwamba agizo hilo limetolewa na waziri wa fedha wa Rwanda kwa mdomo na
kuelezea hali ilivyo sasa.
Ndani
ya bunge, baada ya kamati za bunge za uongozi na kanuni kukutana
hatimae bunge limeitaka serikali kutoa maelekezo ya kina kuhusiana na
suala la mgogoro kati ya wafanyakazi wa shirika la reli ya Tanzania na
Zambia Tazara ndani ya bunge kwa kueleza kiini cha mgogoro huo na hatua
gani madhubuti zimechukuliwa kuutatua kabla ya mkutano huu wa 12 wa
bunge kumalizika.
0 comments:
Post a Comment