BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DAWA YA MIFUGO AINA YA MULTIVITAMIN YATUMIKA KATIKA KUIONGOZEA UKALI KINYWAJI HARAMU CHA GONGO JIJINI DAR ES SALAAM.


Jiko maarufu kama mtambo wa Gongo kikiandaliwa kinywaji hicho.

Dar es Salaam. 
WAKATI Serikali ikiahidi kuongeza nguvu katika vita dhidi ya wauza dawa za kulevya nchini, imebainika kuwa kuna mtandao wa wafanyabiashara wa pombe haramu ya gongo unaopika na kuichanganya na dawa za mifugo ili kuiongezea ukali.

Mtandao huo unaomiliki mitambo ya kupika gongo katika eneo la Mto Kizinga uliopo Dambweni, Kata ya Kilungule, wilayani Temeke, unadaiwa kuchanganya pombe hiyo na dawa ya mifugo aina ya Multivitamin ambayo hutumika kurutubisha wanyama.

Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa dawa hiyo huchanganywa na dawa nyingine ambayo haikufahamika mara moja, kisha kuiweka kwenye gongo ili kuiongezea ukali zaidi.

Wafanyabiashara hao wamekuwa wakipika gongo hiyo katika eneo hilo kwa miaka zaidi ya 10, huku baadhi ya viongozi wa serikali ya mtaa wakitajwa kuwalinda.

Kwa mujibu wa uchunguzi, eneo hilo lina mitambo zaidi ya minne ya kutengeneza gongo na kila mtambo unazalisha pipa moja lenye ujazo wa lita 200.

Uchunguzi ulibaini kuwa kila siku wanazalisha zaidi ya lita 800 za gongo ambayo huuzwa kwa rejareja na jumla. Bei ya rejareja kipimo kinaanzia Sh500 hadi Sh5,000, ambapo bei ya jumla ni Sh38,000 kwa ndoo yenye ujazo wa lita 20.

Kwa mtu anayefika kwa mara ya kwanza eneo hilo atakutana na makundi ya watu wakiwa chini ya miti wakijipumzisha wakati wakisubiri pombe hiyo kuwa tayari, huku wakazi wengine wa eneo hilo wakionekana kuendelea na shughuli zao kwenye bustani za mboga za majani zilizolimwa kando kando ya mto.

Mbali ya kuwa wanalindwa na baadhi ya viongozi wa mtaa, wameweka ulinzi wao wenyewe, kwa kuweka vijana zaidi ya 10 ambao hukaa katika eneo hilo kuhakikisha kuwa mtu anayefika katika eneo hilo wanamtambua.

Ukifika katika eneo ilipo mitambo yao, watu wanaofanya kazi ya kupika ni wacheshi, wanaojaribu kumsalimia kila mpita njia bila ya kuwa na hofu yoyote, huku mmojawao ambaye jina lake halikufahamika mara moja akisema kuwa wao ndio waliotengeneza barabara ya kupita magari inayoingia sehemu hiyo.

Mkazi mmoja wa eneo hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa kuhofia usalama wake, alisema watu hao ndiyo wasambazaji wakubwa wa gongo jijini Dar es Salaam.

“Biashara hii inalipiwa ‘kodi’ kila mwezi, hawa jamaa huchangishana fedha halafu huwapelekea baadhi ya askari ambao huwalinda wasikamatwe, kuna wakati huchanga hadi laki tatu. Vigumu sana kukamatwa,” alisema.Gongo inavyotengenezwa. MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: