BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KINACHOENDELEA SASA HIVI JUMBA LA MADUKA LA WESTGATE MJINI NAIROBI KENYA: VIKOSI VYA USALAMA VYAAKABILIANA NA WANAMGAMBO WA AL-SHABAAB ILI KUWAOKOA MATEKA RAIA WA KENYA WANAOSHIKILIWA NA MGAMBO HAO.

VIKOSI vya usalama vinaendelea na juhudi za kukabiliana na magaidi walioteka nyara baadhi ya wakenya katika jengo la Westgate.
MKUU wa majeshi Meja Jenerali Julius Karangi amesema magaidi hao wanaweza kujisalimisha ikiwa wanataka kwa sababu jeshi litakabiliana nao vilivyo. 

Pia amesema kuwa Kenya inakabiliana na magaidi wa kimataifa.

Ole Lenku anasema kuwa hali ingali tete lakini vikosi vya usalama vya Kenya vinakaribia kuwazingira magaidi hao...Hadi kufika sasa watu 62 wamefariki na wengine zaidi ya 175 kujeruhiwa.

Ole Lenku anasema kuwa wanajeshi kumi wamejeruhiwa na wanapokea matibabu. Pia mateka karibu wote wameweza kuokolewa. Ole Lenku pia amesema kuwa wameweza kuwaua magaidi wawili.

Waziri wa usalama Joseph Ole Lenku anasema kuwa moshi ulitokana na moto uliosababishwa na magaidi walioko ndani ya jengo hilo kujaribu kusambaratisha juhudi za wanajeshi wa Kenya dhidi yao.

Moshi mkubwa ukitoka ndani ya jumba la Westgate14:03 Mkuu wa polisi David Kimaiyo asema kuwa vikosi vya usalama vinakaribia kudhibiti jengo hilo lote na vimeingia ndani kabisa ya jengo hilo kiasi cha kuwaokoa baadhi ya mateka.

Milipuko zaidi yasikika katika jengo hilo.

Mwandishi wa BBC, Idriss Situmaaliye katika eneo la Westgate anasema duru zinaarifu kuwa vikosi vya usalama vya Kenya vinasema kuwa ndivyo vimelipua sehemu ya jengo kujaribu kuingia ndani kabisa ya jengo hilo.

Magari ya Ambulance yaobnekana yakienda katika eneo la shambulizi pamoja na magari ya zima moto. Vikosi vya usalama vinawataka watu kuondoka karibu na eneo la operesheni hiyo ili kuwawezesha kufanya kazi yao

Waathirwa wa shambulizi la Westgate saa 7:49 mchana, Moshi mkubwa mweusi waonekana ukitoka juu katika jengo hilo haijulikani nini kilichosababisha saa 7:19 mchaana Moshi mkubwa unaonekana ukitoka katika jengo la Westgate ambako wapiganaji wa Al Shabaab wanawazuilia mateka wakenya ambao idadi yao haijulikani saa 7:12 mchana Viongozi wa kidini watoa taarifa kulaana kitendo cha Al Shabaab.

SAA 6:30 mchana Milipuko zaidi na milio ya risasi imesikika katika jengo la Westgate huku vikosi vya usalama vikifanya jitahada za misho kuwa

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: