BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KUKITHIRI KWA RUSHWA NDANI YA JESHI LA POLISI, SASA BASTOLA HUMILIKIWA NA VIBAKA NCHINI.

Dar/Mikoani. 
KUKITHIRI kwa rushwa miongoni mwa baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi nchini, kumesababisha silaha ndogondogo hususan bastola kumilikiwa na watu wasio na sifa nchini.
Uchunguzi wa kina wa gazeti hili katika mikoa mbalimbali nchini ikiwamo iliyopo mipakani inaonyesha kuwa, bastola zinamilikiwa na watu bila ya kufuata taratibu na nying
ine zikitumika kwa ajili ya kufanyia uhalifu.
Hivi sasa hata vibaka ambao awali walikuwa wakitumia visu na mbao za misumari kupora mali za watu, sasa wanafanya uhalifu huo kwa kutumia bastola.
Mbali ya vibaka kumiliki bastola, wahamiaji haramu walioko ndani ya mipaka ya Tanzania inayopakana na Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wanadaiwa kuingiza silaha nzito, ambazo zinatumika kwa ajili ya matukio ya kihalifu.
Jinsi silaha zinavyopatikana.
Uchunguzi unaonyesha moja ya njia ambayo imekuwa ikitumika watu wasiokuwa na sifa kupata bastola au bunduki ni kutumia mawakala au baadhi ya maofisa polisi, waliopo katika mikoa mbalimbali ambao huwatafutia vibali vya kumiliki.
Utaratibu wa kawaida ni kwamba waombaji wanaotaka kumiliki silaha ni lazima wajadiliwe katika kamati za ulinzi na usalama za mtaa au kijiji, wilaya na mkoa na kuhojiwa ili kujiridhisha kama mwombaji ana sifa.
Mkoa wa Kilimanjaro
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa baadhi ya vijana wadogo wakiwamo wafanyabiashara, wana vibali vya kumiliki bastola mkoani Kilimanjaro na hawakupitia mchakato huo.
“Unataka kibali cha kumiliki bastola? Una milioni moja na nusu nikuunganishe na jamaa Dar anakufanyia process (mchakato) zote anakuletea kitabu,”alisema kijana mmoja jina tunalihifadhi.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi makao makuu na wale waliopo mikoani, wamegeuza suala la kumilikisha watu silaha kama mradi wa kujitajirisha.
“Tatizo la nchi hii ni corruption (rushwa) kwa sababu unajiuliza hivi hawa vijana wadogo kabisa wanamiliki bastola na hawakujadiliwa kwenye kikao chochote,”alidokeza mfanyabiashara mmoja.MWANANC HI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: