RAIS JAKAYA MRISHI KIKWETE.
WAKATI sakata la dawa za kulevya likiwa limeichafua Tanzania katika
uso wa kimataifa, orodha ya majina ya wanaohusika na biashara hiyo
ambayo Rais Jakaya Kikwete alidai kuwa nayo, amesema amekwishaip
eleka
kwenye Mamlaka husika.
Rais Kikwete mara kadhaa amekuwa akisema kuwa
anayo orodha ya watu wanaouza dawa za kulevya hapa nchini, hivyo gazeti
hili lilimtafuta kupitia kwa msemaji wake, kufahamu suala hilo
lilikofikia.
Akizungumza na gazeti hili kupitia kwa Msemaji wake, Salvatory
Rweyemamu, Rais Kikwete alisema orodha ambayo alisema anayo
alikwishaikabidhi kwa vyombo husika kwa ajili ya hatua zaidi.
“Rais
atembee nayo mfukoni ya nini ?. Hata Nzowa katika taarifa yake alisema
alipatiwa… wamepewa vyombo husika, Serikali haiendeshwi kwa vyombo vya
habari, kuna vingi vinafanyika bila kutangazwa. Mtafute Nzowa atakwambia
vyema,” alisema Rweyemamu, wakati gazeti hili lilipotaka kufahamu juu
ya orodha hiyo ya Rais ilikofikia.
Orodha ambayo Rais Kikwete
amekuwa akielezwa kuwa anayo, inadaiwa kuwahusisha vigogo mbalimbali
nchini, wakiwemo wabunge, mawaziri na wafanyabiashara wakubwa ambao hata
hivyo imebainika kuwako kwa ugumu wa kuwachukulia hatua, kutokana na
kutokuwa na ushahidi ili kuwabana wahusika.
Kutokana na kauli
hiyo ya Rais kupitia kwa msemaji wake, Gazeti hili liliamua kutafuta
moja ya mamlaka zinazohusika kupambana na dawa za kulevya ili kufahamu
juu ya orodha hiyo iliyokabidhiwa na Rais na hatua ambazo zimechukuliwa.
Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya cha Jeshi la
Polisi, Kamishna Msaidizi (ACP), Godfrey Nzowa, hakukiri wala kukana
kupokea orodha hiyo kutoka Ikulu.
MTANZANIA Jumapili: Kamanda
sisi ni MTANZANIA Jumapili, tumepata taarifa kwamba Ikulu imekupatia
majina ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya, vipi umefikia wapi
katika kuishughulikia ?
NZOWA: “Kutoka wapi? Mimi napata kutoka
sehemu mbalimbali, tunakuwa na watu ambao tunakamata na tunawapekua,
ikithibitika tunawapeleka mahakamani
Na hivi karibuni nimepatiwa orodha ya watu 261 wanaodaiwa kufanya biashara hiyo, lakini katika upekuzi wetu hatukukuta kitu.
MTANZANIA Jumapili: Kwa hiyo hao mliowapekua ndiyo orodha mliyopatiwa kutoka Ikulu?
Nzowa: Siwezi kutaja moja kwa moja kwa sababu ninapokea orodha kutoka sehemu mbalimbali, kwa hiyo si salama kutaja jina la mtu.
Siwezi
ku ‘mention’ kuwa ni Ikulu ama nani. Ushahidi wa moja kwa moja haupo,
lakini wa kimazingira upo, tulipeleka kiapo ili washitakiwe Mahakamani.
Kwa mujibu wa Nzowa, wengine zaidi ya 260 waliopatikana na ushahidi wamefunguliwa kesi katika mahakama za hapa nchini.
Hivi
karibuni katika Bunge linaloendelea Dodoma, kuliibuka hoja ya kuitaka
serikali kutaja orodha ya wanaodaiwa kuhusika na biashara ya dawa za
kulevya, ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na
Bunge), William Lukuvi, alishindwa kufanya hivyo.
Badala yake,
Lukuvi alisema baadhi ya majina ya wabunge yametajwa miongoni mwa watu
wanaoshukiwa kujihusisha na biashara hiyo na kwamba angetaja majina,
Bunge lisingebaki salama.
Lukuvi alisisitiza kuwa serikali haiwezi kuwataja hadharani kwa haraka, kwani inaogopa kukurupuka na kushindwa mahakamani.
Hata
hivyo, Lukuvi alisema ukubwa wa biashara hiyo hapa nchini
unadhihirishwa na idadi ya Watanzania 274 waliokamatwa kati ya mwaka
2008 hadi Julai, mwaka huu kwa kosa la kujihusisha na dawa za kulevya
katika nchi mbalimbali za nje.
Pamoja na kukamatwa kwa Watanzania
hao nje ya nchi, wageni 31 wanashikiliwa mahabusu katika Magereza ya
Keko na Ukonga, Dar es Salaam, ambao ni raia wa Iran, Pakistan, Senegal
na Afrika Kusini.
Sakata la dawa za kulevya nchini lilitikisa
zaidi baada ya kukamatwa kwa wasichana wawili, Agness Gerald (25) na
Mellisa Edward (24) katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo, Afrika
Kusini, wakitokea Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, (JNIA) wakiwa na
dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine kilo 150, zenye thamani
ya Sh. bilioni 6.8 za Tanzania.
Hatua hiyo ilimlazimisha Waziri
wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kuwafukuza kazi wafanyakazi wa
JNIA, wanaodaiwa kuhusika na upitishwaji wa mzigo huo, huku baadhi ya
watendaji wakihamishwa vituo vyao vya kazi.
Moto huo uliowashwa
na Mwakyembe, ulikuja baada JNIA kutajwa kuwa moja ya chochoro kubwa za
kupitisha dawa hizo, hali ambayo pia imeshuhudia Jeshi la Polisi
kuwaondoa kwa kuwahamisha vituo vya kazi, Kamanda wa Polisi wa Viwanja
vya Ndege, Kamishna Msaidizi (ACP) Deusdedit Kato na Mkuu wa Upelelezi
wa Viwanja hivyo, David Mwafwimbo. MTANZANIA
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / KUMBE RAIS JAKAYA KIKWETE TAYARI AMEPELEKA MAJINA YA WAFANYA BIASHARA WA UUZAJI NA USAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA, KAMANDA NZOWA MAJINA YAPO 261, ILA KUYATAJA KAZI KWELI KWELI !!!.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment