BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MSAMVU TERMINAL, HIACE TERMINAL ZATINGA FAINALI YA LIGI YA NANE NANE CUP 2013 NI BAADA YA KUZIKUNG'UTA KAIZER CHIEF NA KABAANG FC KATIKA UWANJA WA SABASABA MJI KASORO BAHARI.

Mchezaji wa Kaizer Chief Moses Kachonge kulia akipiga mahesabu ya kumtoka Khalidi Zoro wa Msamvu Terminal wakati wa mchezzo wa nusu fainali ya ligi ya Nane Nane Cup 2013 katika uwanja wa Sabasaba Manispaa ya Morogoro ambapo katika mchezo huo Kaizer Chief ilikubali kipigo cha bao 2-0. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM

Na Juma Mtanda, Morogoro.
MABAO mawili yaliyopachikwa wavuni na washambuliaji, Willberd Palike na Faraji Makongoro yaivusha timu ya soka ya Hiace Terminal kutinga fainali ya ligi ya Nane Nane Cup 2013 baada ya kuilalua Kabaang FC katika mchezo mkali wa nusu fainali ya ligi hiyo uliochezwa katika uwanja wa Sabasaba Manispaa ya Morogoro.

Mshambuliaji Willberd Palike alifunga bao la kuongoza kwa kichwa katika dakika ya tano kufuatia mpira wa kona uliochongwa na Kelvin Kong’oa na kuruka juu na kujaza mpira kimiani na kumshinda kipa Jackson Anthony alisijue la kufanya.

Dakika ya 32, Faraji Makongoro alifunga bao la pili baada ya kumlamba chenga mlinzi wa Kabaang FC, Peter Mjata na kufumua shuti kimo cha mbuzi na kujaza mpira katika nyuvu na kwenda mapumziko Hiace Terminal wakiongoza bao hizo 2-0.

Kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko kwa lengo la kuongeza idadi ya mabao huku nyingine ikitaka kusawazisha mabao lakini hata hivyo mabadiliko hayo hayakusaidia kubadilisha matokeo ya mchezo huo uliomalizika kwa Kabaang FC kukubali kipigo cha bao 2-0.

Katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo itazikutanisha timu zinazotoka eneo moja la kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Msamvu Manispaa ya Morogoro za Msamvu Terminal dhidi ya Hiace Terminal, ambapo mashabiki wa soka katika Manispaa hiyo itashuhudia mbabe wa ligi hiyo ya Nane Nane Cup 2013.

Timu ya Hiace inaundwa na wachezaji wanaotokana na madereva wa daladala na makondakta zinazofanya kazi za kusafarisha abiria kati ya Mjini na Kihonda wakati Msamvu Terminal yenyewe inaundwa na mawakala wa kukatisha tikiti za mabasi ya mikoa na wapiga debe.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: