Alifungua makanisa zaidi ya 4,600 ya EAGT ndani na nje ya Tanzania, ikiwemo Zambia, Malawi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC).
Lakini cha kushangaza ana nyumba moja tu tena aliyojengewa na waumini wake.
Ni vigumu kuzungumzia historia ya vuguvugu la uanzishaji makanisa nchini, pasipo kumtaja Askofu Moses Kulola.
Askofu Kulola anajulikana na wengi kama mtu aliye na nia ya dhati kutangaza neno la Mungu, kutokana na kile kinachoonekana wazi kwamba hakujilimbikizia mali kama ambavyo tunaona baadhi ya watumishi wa Mungu siku hizi wanavyomiliki majumba, benki na hata magari ya milioni ya shilingi.
Hali halisi.
Kwa namna inavyoonekana nchini, ni kama kuna kundi kubwa la watumishi wanaohubiri kwa lengo la kushibisha matumbo yao zaidi; Hawana mpango thabiti wa kusaidia yatima wala maskini, badala yake waumini ndio wanaonyonywa kwa kutoa zaka na sadaka ambazo baadhi yake hata matumizi yake yamekuwa yakizua maswali.
Utumishi wa Mungu na mali.
“Hakuna shaka kwamba kama kila nyumba ya ibada Tanzania ingekuwa na mpango thabiti wa kusaidia watu maskini, yatima na watu wengine wenye hali ngumu, hali ya maisha ingekuwa nzuri zaidi kwa wengi.

Lakini wapi, baadhi ya watumishi wako ‘bize’ kujaza matumbo, wanaendesha magari ya kifahari yenye thamani ya mamilioni ya shilingi badala ya kutumia fedha hizo kutangaza neno la Mungu au kusaidia wasiojiweza,” anasema Charles Mtanga, mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam.
Mtanga anawashauri viongozi wa nyumba za ibada kuwa na mkakati wa kusaidia yatima na watu wengine wasio na uwezo, huku wakiendelea kutangaza neno la Mungu, ili wote waweze kuufurahia ulimwengu.
Utanuzi wa huduma.
Kwa mujibu wa Askofu wa EAGT Sengerema, Joshua Wawa, Askofu Kulola alizaliwa Juni 2, 1928 katika Kijiji cha Nyahonge wilayani Kwimba mkoani Mwanza. Ameacha mjane, watoto 10, wajukuu 44 na vitukuu 16.
Katika uhai wake, Askofu Kulola alifungua makanisa 4,600 ya EAGT ndani na nje ya Tanzania, ikiwemo Zambia, Malawi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC) na ameacha wosia kwamba makanisa yafunguliwe kadiri inavyowezekana.
Hata hivyo, licha ya kuwa na wingi wote huo wa makanisa, Askofu Kulola anamiliki nyumba moja iliyoko mkoani Mwanza aliyojengewa na waumini.Askofu Moses Kulola.

Wakati Askofu Kulola akifariki dunia katika mazingira hayo naye Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl Julius Nyerere hakuwa na tabia kujilimbikizia mali. MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment