KIJANA mbakaji ambaye alifungwa jana anasubiria vipimo kubaini kama ameathirika na virusi vya ukimwi kutoka kwa muathirika aliye mbaka.
Richard
Thomas, mwenye umri wa miaka 27, alianguka chini pale polisi
walipomtaarifu kuhusu hali ya afya ya mwanamke huyo na anasubiria
kusikia kama ameathirika na virusi hivyo visivyotibika.
Thomas,
mkazi wa Leigh huko Greater Manchester, alimfahamu mwanamke huyo na
alijua kwamba ana ugonjwa mwingine lakini hakuwa akijua kuhusu virusi
vya ukimwi. Mahakama ilielezwa alishitushwa pale alipotakiwa kupelekwa
hospitali, Mahakama Kuu ya Liverpool ilielezwa.
Alijipeleka nyumbani kwake katikati ya usiku na mwanamke huyo akazinduka usingizini na kukuta Thomas akimbaka.
"Alitulia na hakuna aliyemwongelesha mwenzake. Alipangisha kaptula yake na kuondoka," alisema mwendesha mashitaka Harry Pepper.
"Alikamatwa
na kuhojiwa na alisema alikuwa amelewa kupita kiasi, kutumia cocaine na
kurukwa akili na hakuweza kukumbuka tukio hilo," aliongeza.
Wakili
wake, Virginia Hayton, alisema kwamba bado hawezi kukumbuka shambulio
hilo lakini alipoelezwa kuhusiana na hilo alisema kwamba mwanamke huyo
'hawezi kusema uongo, anaeleza ukweli. Kama anasema nimefanya hivyo,
basi nimefanya'.
Akimfunga
Thomas miaka mitano na miezi minne jela Jaji Mark Brown alisema kwamba
amefanya 'kosa hili lisilopendeza' wakati mwanamke huyo akiwa amelala
fofofo, akiwa amemeza vidonge vya usingizi, na ilimwacha akiwa mwenye
mateso na wasiwasi.
Pia
alimwamuru Thomas kusaini Rejista ya Wahalifu wa Kujamiiana kwa maisha.
Thomas alipatikana na hatia ya kumbaka mwanamke huyo Julai 20 mwaka
huu.
Hayton
alisema kwamba Thomas, ambaye hapo kabla alishawahi kutiwa hatiani
lakini si kwa makosa ya ubakaji, 'katili' na 'hawezi kuelewa kwanini
alifanya vile na inamsumbua mno'.
Alisema
kwamba alianza kutumia bangi akiwa na umri wa miaka tisa, kunywa pombe
kupita kiasi akiwa na umri wa miaka 11, kutopea dawa za kulevya hadi
kufikia kurukwa akili na cocaine akiwa na umri wa miaka 13 na aliwekwa
chini ya uangalizi maalumu mwaka uliofuata.
Amekuwa
akijaribu kuwasiliana na familia yake lakini hawataki kufanya chochote
kumsaidia na sasa atakuwa mbali na mpenzi wake na binti yao mdogo na
mabinti zake wengine wawili wakubwa aliowapa katika mahusiano yake ya
awali.
Hayton
aliieleza mahakama hiyo kwamba Thomas hawezi kupata majibu ya vipimo
vyake vya virusi vya ukimwi hadi Ijumaa na amekuwa na hofu kubwa ya
matokeo hayo.
"Ni kosa lake mwenyewe, kama asingefanya kosa hili asingejiweka mwenyewe mahali hapa."
0 comments:
Post a Comment