DODOMA.
MUSWADA wa Sheria ya Kura ya Maoni wa mwaka 2013 uliokuwa ujadiliwe katika mkutano wa 12 wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma, umeondolewa na sasa utajadiliwa Bunge lijalo.
MUSWADA wa Sheria ya Kura ya Maoni wa mwaka 2013 uliokuwa ujadiliwe katika mkutano wa 12 wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma, umeondolewa na sasa utajadiliwa Bunge lijalo.
Habari za uhakika zilizopatikana jana, zilisema
kwamba kuahirishwa huko kumetokana na wajum
be wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge wanaotoka Zanzibar kupinga vikali kura ya maoni kupigwa visiwani humo kwa kuwa tayari huko kuna sheria hiyo.
be wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge wanaotoka Zanzibar kupinga vikali kura ya maoni kupigwa visiwani humo kwa kuwa tayari huko kuna sheria hiyo.
Muswada huo ulikuwa ujadiliwe na wabunge katika
kikao cha Bunge kinachoendelea ukitanguliwa na Muswada wa Sheria ya
Marekebisho ya Sheria ya mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013.
“Ukisoma huu Muswada unasema kura hiyo itapigwa
Tanzania Bara na Zanzibar sasa sheria hii ina apply vipi (inatumikaje)
Zanzibar wakati kule tuna sheria yetu tayari?” alihoji Mbunge mmoja wa
Zanzibar.
Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alipoulizwa jana,
alithibitisha kuondolewa kwa muswada huo wa kura ya maoni kusema na
utakaojadiliwa ni ule wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba pekee.
“Bunge litaahirishwa Ijumaa (keshokutwa) na ni
kweli huo Muswada wa Kura ya Maoni umeondolewa kwa sababu bado uko
kwenye ngazi ya kamati,” alisema Joel.
Alipoulizwa sababu za kuondolewa kwa muswada ambao
ulishaingizwa kwenye ratiba ya Bunge, alitaka swali hilo aulizwe Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.
Waziri Lukuvi alithibitisha kuondolewa kwa muswada huo na kusema utajadiliwa katika Mkutano wa Bunge wa Oktoba.
“Ni kweli muswada huu hautajadiliwa na Bunge hili
bado kuna mashauriano yanaendelea kati ya SMZ (Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema.
Kwa upande wake, Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alisema wabunge wa Zanzibar ndiyo
waliokwamisha muswada huo kutokana na mgongano wa sheria.
“Wao wanasema masuala ya kura ya maoni siyo ya
Muungano kwa sababu wao tayari wana sheria yao ya kura ya maoni. Sasa
wanahoji inakuwaje sheria hii itumike tena hadi Zanzibar? Huu ni
mgongano,” alisema.
Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki
(Chadema), alisema tangu mwanzo aliliona suala hilo na kuitahadharisha
Kamati ya Bunge kwamba mapendekezo hayo yana upungufu. MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment