Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa jengo la
madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa
na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano na Serikali
ya Oman,huko Mbweni Nje ya Mji wa Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mshauri wa Mambo ya Afya,Wizara ya Afya ya Oman,Dr.Sayeed
Sultan Bin Yarub Bin Qaatan Al- Busaid,wakikata utepe kama ishara ya ya
uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya
Afya,lililogharamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano
na Serikali ya Oman,huko Mbweni Nje ya Mji wa Unguja leo.
R
ais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa ushauri wakati alipotembelea moja ya madarasa
ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,huko mbweni baada ya kuyazindua
rasmi leo,ambayo yamejengwa kwa ufadhili ya Serikali ya Oman kwa
kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa nasaha zake,baada ya kuyazindua rasmi
madarasa ya chuo hicho leo ,hapo chuoni Mbweni,Mkoa wa Mjini Mgharabi
Nje ya Mji wa Unguja,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea risala ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,kutoka
kwa Mkuu wa Chuo hicho Dk. Haji Mwita,baada ya kuyazindua Rasmi
madarasa ya Kusomea,yaliyojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Oman,na
ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akitoa hutuba yake kwaWananchi na wanafunzi (hawapo pichani) wakati wa Sherehe za Uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa
na Serikali ya Oman kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar,huko Mbweni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo,(kushoto) Waziri
wa Afya Juma Duni Haji,na Mshauri wa Mambo ya Afya,Wizara ya Afya ya
Oman,Dr.Sayeed Sultan Bin Yarub Bin Qaatan Al- Busaid,(kulia).
Mshauri wa Mambo ya Afya,Wizara ya Afya ya Oman,Dr.Sayeed Sultan Bin Yarub Bin Qaatan Al- Busaid,akitoa salamuzake
wakati wa sherehe za uzinduzi wa madarasa mapya ya kusomea katika Chuo
cha Taaluma za Sayansi ya Afya,yaliyojengwa na Serikali ya Oman,na
ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.(Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.)
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment