Nyumba ya milele ya marehemu Venance George Mhangilwa aliyefariki dunia Septemba 26 katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kisha mwili wake kusafirishwa juzi Septemba 27 saa 1 usiku kutoka Morogoro kwenda kijiji cha Bukoli Geita baada ya shughuli ya kuaga mwili kufanyika nyumbani kwake mtaa wa Tubuyu kata ya Tungi, hapa ni ardhi ya kijiji cha Bukoli muda mfupi kabla ya mazishi yake yaliyofanyika jana alasiri kijijini hapo.
Jeneza lenye mwili wa Mkuu wa waandishi wa habari gazeti la Mwananchi Communication LTD mkoa wa Morogoro Venance George Mhangilwa (40) mara baada ya kuwasili katika makaburi yaliyopo kijiji cha Bukoli Geita kwa ajili ya mazishi, Mwenyezi mungu ampumzishe mahala pema peponi mpendwa wetu, Amina.

0 comments:
Post a Comment