ZANZIBAR.
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Sophia Simba, ameshutumiwa kwa kitendo chake cha kumteua Salama Aboud Talib kwenye nafasi ya Naibu Katibu Mkuu, wakati anatuhumiwa kwa ufisadi wa mali za jumuiya.
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Sophia Simba, ameshutumiwa kwa kitendo chake cha kumteua Salama Aboud Talib kwenye nafasi ya Naibu Katibu Mkuu, wakati anatuhumiwa kwa ufisadi wa mali za jumuiya.
Taarifa za ndani ya jumuiya zilidai kuwa uteuzi wa
Salama, anayeshika wadhifa huo kwa upande wa Zanzibar, umekiuka azimio
la Kamati ya Utekelezaji lililotaka achung
uzwe kutokana na tuhuma za ufisadi wa mali za UWT upande wa visiwani.
uzwe kutokana na tuhuma za ufisadi wa mali za UWT upande wa visiwani.
Salama kabla ya uteuzi huo wa sasa, alikuwa
akishika wadhifa huo lakini katika awamu hiyo ya uongozi wake kulikuwa
na tuhuma za ufisadi wa mali za jumuiya na kwamba Mwenyekiti Sophia
Simba amemteua wakati akiwa bado anachunguzwa.
Malalamiko hayo yamejitokeza baada ya kukamilika
kwa Baraza Kuu la UWT Taifa lililokutana katika ukumbi wa hoteli ya
Dodoma, Agosti 26 mwaka huu wakiwa na ajenda ya kumwidhinisha Katibu
Mkuu na manaibu wake Bara na Zanzibar.
Wakizungumza na gazeti hili kwa masharti ya
kuhifadhiwa majina yao, baadhi ya wajumbe wa baraza hilo walidai Salama
hakustahili kurejeshwa kwenye nafasi hiyo, kwa kuwa tume ya uchunguzi
dhidi yake bado haijakamilisha kazi yake.
Mmoja wa wajumbe alidai azimio la Kamati ya
Utekelezaji iliyokutana mwezi uliopita, iliundwa tume ya kuchunguza
tuhuma za ufisadi za mali za UWT Zanzibar dhidi ya Salama.
Alisema tume hiyo inawajumuisha Dk Aisha Kigoda,
Zarina Madabida, Zainab Mwamidi na Mwanaidi Kassim ambao miongoni mwao
walitakiwa kuchagua mwenyekiti wa tume hiyo ili kukamilisha kazi ya
uchunguzi na kuwasilisha ripoti.
“Tulipokwenda kwenye Baraza Kuu tulikuwa na ajenda
ya kumthibitisha Katibu Mkuu, Amina Makilagi na Naibu wake Grace Kiwele
cha kushangaza mwenyekiti amepitisha na kumthibitisha Salama Aboud
Talib, kinyume na maazimio ya kamati ya utekelezaji,”alisema mjumbe
mmoja ambaye ni kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM.
Alipoulizwa juu ya suala hilo, Sophia Simba
alithibitisha kuteuliwa kwa Salama kushika wadhifa huo na kueleza kuwa
umefanyika kwa kuzingatia utendaji na uchapakazi wake wa mhusika.
“Salama ataendelea kuwa Naibu Katibu Mkuu
Zanzibar, uwezo wake ni mkubwa kiutendaji, tuhuma kama zipo ni kwa UWT
kama jumuiya na si kwake tu,”alisisitiza mwenyekiti huyo.
Sophia alisema kufanyika kwa uteuzi huo
hakusitishi mambo mengine kutoendelea ikiwamo tuhuma zinazolalamikiwa
kufanyiwa uchunguzi.
Inaelezwa sababu ya kuundwa kwa tume ni baada ya
kujitokeza tuhuma kuhusu mali za UWT, zikiwamo nyumba za kuoka mikate
huko Unguja na Pemba na vitegauchumi vingine kutoinufaisha jumuiya hiyo. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment