Watu wakitafuta usalama wao wakati wanajeshi walipoingia kwenye maduka ya kifahari ya westgate kufanya operesheni.
KENYA imesema mateka wachache wamebaki ndani ya maduka ya kifahari ya Westage Mall yaliyovamiwa na wanamgambo wa kiislamu wa Al- shabab Jumamosi ambapo dazani za watu wameuwawa.
Kundi la kigaidi la wanamgambo la Al- shabab limedai kuhusika na shambulizi likisema kuwa linajibu kuhusu majeshi ya Kenya yaliyoko katika operesheni nchini Somalia.
Majeshi ya Kenya yalianza kufanya mashambulizi Jumapili jioni katika maduka hayo ya kifahari ya Westage Mall kuokoa watu waliokuwa wamejificha au kushikiliwa mateka na watu wenye silaha.
Waziri wa mambo ya ndani Joseph Ole Lenku, aliuambia mkutano wa waandishi wa habari Jumatatu kwamba vikosi vya Kenya sasa vinadhibiti kila ghorofa la jengo hilo na tayari yameokoa takriban mateka wote waliokuwa wamebaki ndani.
Amesema watu wawili waliokuwa na silaha waliuwawa katika operesheni za kijeshi zinazoendelea na wanajeshi 10 wa vikosi vya usalama wamejeruhiwa.
Lenku alizungumza kwa karibu dakika 90 baada ya mashahidi kusikia milipuko mikubwa iliyokuwa inatokea kwenye Mall ikifuatiwa na milio ya bunduki. Moshi mkubwa mweusi bado unaendelea kufuka kutoka kwenye Mall baada ya milipuko hiyo. Lenku anasema wanamgambo walichoma moto magodoro ili kuvuruga hali.
Amesema watu 62 wameuwawa tangu shambulizi hilo lilipozuka Jumamosi ambapo na Shirika la msalaba mwekundi la Kenya limetoa idadi ya vifo kuwa ni 69 huku 175 wakiwa wamejeruhiwa na takriban watu wengine 65 hawajulikani walipo. http://www.voaswahili.com
0 comments:
Post a Comment