BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAKATI TANZANIA MHE MBOWE AKIONDOLEWA BUNGENI, WENZAO WA UPINZANI NCHI KENYA WENYEWE WAJIONDOA KISA MJADALA WA ICC..

RAIS UHURU KENYATTA.

BAADHI ya wabunge wa upinzani nchini Kenya wameondoka bungeni wakati mjadala mkali ukiendelea kuhusu kuunga mkono au kupinga nchi hiyo kujiondoa kutoka katika mahakama ya kimataifa ya ICC.

Wabunge hao wameondoka bungeni baada ya kusema kuwa kamwe hawataungana na upande wa serikali kuunga mkono hoja hii ya kujiondoa kutoka katika mahak
ama ya ICC. Ni kutokana na kuwa kwamba upinzani una idadi ndogo zaidi ya wabunge bungeni.Naibu rais wa Kenya William Ruto.

Naibu kiranja wa wabunge walio wachache bungeni Jakoyo Midiwo, alisema kuwa wabunge wa upande wa serikali wanaotetea hoja hii ya kujondoa Hague watakuja kujuta. 

Mjadala huu unatokana na hatua ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kukabiliwa na kesi za uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama hiyo wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007-2008.

Hatua hii ya wabunge inakuja zaidi ya wiki moja kabla ya kuanza kwa kesi dhidi ya naibu Rais wa Kenya Williiam Ruto kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2008.

Ruto anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Rais Uhuru Kenyatta pia anatarajiwa kufika katika mahakama hiyo mwezi Novemba kwa kesi dhidi yake.

Wawili hao wanashtakiwa kwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mwishoni mwa mwaka 2007.

Msemaji wa ICC ameambia BBC kuwa kesi hiyo itaendelea hata ikiwa Kenya itajiondoa kwenye mkataba wa Roma uliopelekea kuanzishwa kwa mahakama hiyo.

Bwana Fadi El Abdallah, alisema kuwa itachukua karibu mwaka mmoja kwa mchakato wa nchi yoyote ile kujiondoa kutoka katika mahakama ya ICC na hii bila shaka inaathiri tu kesi zilizokuwa mbele ya mahakama hiyo kwa wakati huo.

Hii ni hatua ya dharura inayochukua serikali kujitoa katika Mkataba wa Roma wa mahakama hiyo ulioidhinishwa na Umoja wa mataifa mnamo tarehe 17 July, mwaka1998.

Kenya inataka kutoa mfano wa kuwa nchi ya kwanza Afrika kuchukua hatua hiyo licha ya kwamba uamuzi huu hautoathiri kwa namna yoyote kesi zinazoendelea sasa katika mahakama ya ICC.

Mahakama hiyo ya kimataifa imesema kwamba kesi hizo zitaendelea hata iwapo Kenya itajitoa.

Imesema itaichukua Kenya kiasi ya mwaka mmoja kabla ya kukubaliwa ombi hilo la kutaka kujiondoa katika mkataba wa Roma na hilo litaathiri tu kesi zitakazozuka baada ya muda huo.

Haya yanajiri wakati makamu wa rais William Ruto anatarajiwa kuondoka Kenya kueleka Hague Uholanzi wiki ijayo kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadaamu katika mahakama hiyo ya ICC, kesi inayoanza tarehe 10 mwezi huu.

Wote wameshtakiwa kwa kuhusika katika ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.Kesi dhidi ya rais Uhuru Kenyatta inatarajiwa kuanza tarehe 12 mwezi Novemba. BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: