BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ZIFAHAMU SABABU ZA KUWA NA VIJIWE KATIKA FIGO ZA BINADAMU NA ATHARI ZAKE KIAFYA.

Kwa kiasi kikubwa, vijiwe husababishwa na kukosekana kwa usawa wa maji, madini na tindikali mwilini, ambayo kitaalam huitwa electrolyte imbalance.
FIGO YENYEWE NDIYO HII.
 
Ni tatizo ambalo linasumbua wengi lakini ambalo halifahamiki vizuri.
Tumesikia habari mbalimbali zinazohusu tatizo hili na dhana mbalimbali ambazo zimekuwa zikijengwa.
Hata hivyo, baadhi ya watu hukumb
wa na tatizo la kuwa na vijiwe katika figo na mfumo wa mkojo kwa jumla.
Mawe haya hutokana ama madini, chumvi au tindikali mbalimbali zinazotolewa mwilini.  Nchini Tanzania, baadhi ya wagonjwa hushtuka wakielezwa wana tatizo hili wakidhani labda wamerogwa, ila jambo la msingi watambue  hili ni tatizo la kiafya.
Aina za mawe katika figo
Aina za vijiwe katika figo ni pamoja na vijiwe vya calcium oxalate, vijiwe vya tindikali ya uriki (uric acid), vijiwe vya struvite (magnesium, ammonium na phosphate)
Sababu za vijiwe katika figo
Kwa kiasi kikubwa, vijiwe husababishwa na kukosekana kwa usawa wa maji, madini na tindikali mwilini, ambayo kitaalamu huitwa electrolyte imbalance.
Kuna magonjwa kadhaa ambayo husababisha kwa kiasi kikubwa kutokea kwa hali hii kama ugonjwa wa utindikali kwenye mirija ya figo, matatizo kwenye tezi za shingo, kukojoa chumvi chumvi za oxalate kupita kiasi na hali ya nyama za figo kuwa tepetepe.
Nani yupo hatarini?
Tatizo hili huwapata zaidi watu walio na historia ya familia zao kuwa na vijiwe kwenye figo, walio na umri kuanzia miaka 40 au zaidi,  ingawa tatizo hili linaweza kutokea katika umri wowote.
Pia, linaweza kuwapata wanaume zaidi kuliko wanawake, wana  upungufu wa maji mwilini, kwa lugha rahisi wale wasiopenda kunywa maji katika kiwango kinachoshauriwa. MWANANCHI.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: