BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ABIRIA 20 WAFARIKI DUNIA WAKIWEMO WATOTO 15 KATIKA MTO NIGER KUFUATIA BOTI WALIOKUWA WAKISAFIRIA KUPASUKA.


WATU Ishirini wamefariki dunia, wakiwemo watoto 15 , baada ya boti waliyokuwemo kupasuka usiku wa kuamkia leo kwenye mto Niger karibu na mji wa Mopti nchini Mali maafisa wamesema na kuongeza kuwa watu 23 hawajulik

ani walipo na wengine 120 wamenusurika.

Kamanda Dramane Diallo, kutoka timu ya huduma ya uokozi ameiambia AFP kuwa chanzo cha kupasuka kwa boti hiyo bado hakijafahamika na kwamba uchunguzi unaendelea. 


Afisa mwandamizi wa serikali kamanda Naman Keita, amethibitisha idadi ya watu 20 kupoteza maisha na kuongeza kuwa watoto 15 ni miongoni mwa waliopoteza maisha ambapo zoezi la kutafuta manusura lilisitishwa usiku huo na litaanza tena leo asubuhi. 


Kamanda Dramane pia amesema boti hiyo ilijazwa na mizigo kupita kiasi jamboa ambalo huenda likawa miongoni mwa sababu za kupasuka kwa boti hiyo.

Dramane ameongrza kuwa shughuli za uokozi za kikosi cha Mali zimefanyika kwa ushirikiano na wakazi wa mji wa Koubi pamoja na boti zingine zilizokuwa zikipita. CHANZO kiswahili.rfi.fr


Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: