Jamal
Emil Malinzi ndiye Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF). Malinzi ameshinda wadhifa huo katika uchaguzi wa Kamati ya
Utendaji ya TFF uliofanyika juzi (Oktoba 27 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam.
ALIIBUKA na ushindi wa kura 73 dhidi ya mpinzani wake pekee Athuman Jumanne
Nyamlani aliyepata kura 52. Nafasi ya Makamu wa Rais imetwaliwa na
Wallace Peter Karia aliyepata kura 67 na kuwashinda Ramadhan Omari
Nassib kura 52 huku Imani Omari Madega akipata kura sita.
Akizungumza
mara baada ya kuchaguliwa, Rais Malinzi ametaka ushirikiano kutoka kwa
wadau wote akiwemo mpinzani wake Nyamlani katika kuhakikisha mpira wa
miguu nchini unasonga mbele.
Pia
ametoa msamaha kwa watu wote waliokuwa wamefungiwa kuanzia ngazi ya
wilaya, mkoa na TFF. Msamaha huo hauwahusu wale waliofungiwa kwa makosa
ya rushwa au kupanga matokeo. Vilevile msamaha huo hauhusu adhabu
zilizotolewa katika ngazi ya klabu.
Rais Malinzi pia amevunja kamati zote za TFF ambapo ataziunda upya kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji.
Kwa
upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji walioshinda ni Kalilo Samson
(Kanda namba 1- Geita na Kagera) aliyepata kura 102 za ndiyo na 17 za
hapana. Kanda namba 2- Mara na Mwanza, mshindi ni Vedastus Lufano
aliyepata kura 51 dhidi ya Jumbe Odessa Magati (11), Mugisha Galibona
(24), na Samwel Nyalla (39).
Epaphra
Swai ndiye mshindi wa Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu kwa kura 63
dhidi ya Mbasha Matutu aliyepata 61. Kanda namba 4- Arusha na Manyara
mshindi ni Omali Walii Ali aliyepata kura 53 dhidi Elley Mbise (51),
Ally Mtumwa (19).
Kanda namba 4- Kigoma na Tabora, mshindi ni Ahmed Idd Mgoyi aliyepata kura 92 dhidi ya 28 za Hamisi Yusuf Kitumbo.
Ayubu
Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo ameshinda Kanda namba 6- Katavi na
Rukwa kwa kura 73 dhidi ya Ayubu Nyaulingo aliyepata 52. Ayoub Shaibu
Nyenzi ndiye mshindi wa Kanda namba 7- Iringa na Mbeya kwa kupata kura
59 na kuwapiku David Samson Lugenge (8), John Exavery Kiteve (12) na
Lusekelo Elias Mwanjala (46).
Kanda
namba 8- Njombe na Ruvuma inawakilishwa na James Patrick Mhagama
aliyepata kura 93 dhidi ya 31 za Kapteni mstaafu Stanley William
Lugenge. Athuman Kingombe Kambi ndiye mshindi wa Kanda namba 9- Lindi na
Mtwara kwa kura 84 akiwazidi Francis Kumba Ndulane (30) na Zafarani
Mzee Damoder (11).
Hussein
Zuberi Mwamba ametetea ujumbe wa Kanda namba 10- Dodoma na Singida kwa
kura 63 akiwapiku Stewart Masima (58) na Charles Komba (4). Geofrey
Irick Nyange ameshinda Kanda namba 11- Morogoro na Pwani akipata kura 78
dhidi ya Juma Pinto (26), Farid Nahdi (14), Riziki Juma Majala (5) na
Twahil Twaha Njoki (2).
Kanda
namba 12- Kilimanjaro na Pwani, Khalid Abdallah Mohamed ndiye
aliyeibuka kidedea kwa kura 69 dhidi ya 54 za mpinzani wake Davis Elisa
Mosha. Kidao Wilfred Mzigama ameshinda Kanda namba 13- Dar es Salaam kwa
kupata kura 60 dhidi ya wapinzani wake Muhsin Said Balhabou (50), Omar
Isack Abdulkadir (10) na Alex Crispine Kamuzelya (4).
http://www.shaffihdauda.com
0 comments:
Post a Comment