BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BAADA YA KUPIGWA RISASI MBILI JUZI NA MPENZI WAKE, MWANDISHI NA MTANGAZAJI WA KITUO CHA TELEVISHENI, UFOO SARO SASA AFYA YAKE YAANZA KUIMARIKA.

Kaka wa marehemu Anthery Mushi aliyemuua mkwewe, kumjeruhi mzazi mwenzake, Ufoo Saro na kujipiga risasi, Silva Andrea akizungumza jijini Dar es Salaam jana, kuhusu taratibu za mazishi ya mdogo wake anayetarajiwa kuzikwa wiki hii, Uru, Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro. Wa pili kushoto ni kaka mwingine wa marehemu, Isaya Mushi.Picha na Michael Jamson.

DAR ES SALAAM.
HALI ya mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro aliyejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi mbili juzi huko Kibamba, Dar es Salaam inazidi kuimarika na jana alizungumza na gazeti hili na kusema; “Sijambo, naendelea vizuri.”
Ufoo, ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, hata hivyo, anazungumza kwa shida kutokana na kukabiliwa na maumivu baada ya kufanyiwa upasuaji juzi.

Mwandishi huyo amehamishiwa katika wodi ya upasuaji wa moyo huku kiongozi wa wodi hiyo, ambaye alikataa jina lake kuandikwa gazetini, akieleza kuwa walimhamishia huko ili apate muda zaidi wa kupumzika.

“Watu wanakuja kwa wingi kumjulia hali, tuliona tumhamishe ili apumzike,” alisema kiongozi huyo.

Kabla ya kupelekwa katika wodi hiyo, Ufoo alikuwa katika wodi ya Kibasila na baadaye alihamishiwa katika Chumba cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU).

Ufoo alipigwa risasi na mzazi mwenzake, Anthery Mushi ambaye alijiua baadaye. Pia Mushi anatuhumiwa kumuua mama yake Ufoo, Anastazia Saro wakati wa tukio hilo.

Mazishi ya mama yake Ufoo yamepangwa kufanyika Ijumaa huko Machame mkoani Kilimanjaro.

Ufoo aongea kwa shida
Mara baada ya mwandishi wa gazeti hili jana kuingia
katika chumba alicholazwa Ufoo huku akisindikizwa na wauguzi watatu, mwandishi huyo alitoa mkono wake na kusema; “Njoo hapa unisalimie huku umenishika mkono.”

Huku akionyesha uchovu na kusikia maumivu, alizungumza kwa tabu na kusema; “Sijambo naendelea vizuri.”

Mara baada ya wauguzi hao kumweleza kuwa kati ya waandishi zaidi ya 30 waliofika kumjulia hali ni watatu tu ndiyo walioruhusiwa kumwona alitaka kujua ni kina nani waliobaki nje kwa kuhoji; “Nani hao wako nje.” MWANANCHI.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: