BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BENDERA AKERWA NA WANANCHI WANAOFUNGA BARABARA KWA KUWEKA VIZUIZI KWA KISINGIO CHA KUSHINIKIZA VIONGOZI KUTATUA KERO, DAWA YA TABIA HIYO IPO JIKONI INATOKOTA.





MKUU WA MKOA WA MOROGORO JOEL BENDERA.

Na Juma Mtanda, Morogoro.
MKUU wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera amekerwa na tabia ya baadhi ya wananchi wanaojichukulia hatua ya kuziba barabara kwa kuweka mawe, magogo na wengine kulala barabarani kwa nia ya kushinikisha kutat

uliwa kero zao.

Bendera alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alisema kuwa amehamua kutoa onyo hili kwa wananchi baada ya kuona tabia hizo za kuziba barabara kushamili katika maeneo mengi ya mkoa huo.

“Ni marufuku kwa mtu ama kikundi katika kijiji au mji mkoani hapa kuweka vizuizi barabarani kwa kisingizio cha kupata ufumbuzi wa kero yoyote katika na atayefanya vitendo hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa hata kushtakiwa na vyombo vya dora,”alisema Bendera.

Hivi karibuni kumezuka tabia ya baadhi ya wananchi katika vijiji kuweka vizuizi kama mawe,magogo na hata wengine kulala barabarani ili kuzuia magari yasipite kwa lengo la kushinikiza kutatuliwa kero zao na viongozi wa ngazi za juu,jambo linalosababisha vurugu na hata kupoteza amani.

Alivitaja vijiji ambavyo vimekumbwa na kuwekwa vizuizi barabarani ni mji mdogo wa Dumila, Doma, na Turiani-Dihombo.

Bendera alisema kuwa tabia hiyo ya kuweka vizuizi katika barabara kuu kwa lengo la kushinikiza kiongizi wa ngazi yoyote kutaka atatue kero yake imekuwa ikisababisha madhaara makubwa hasa kwa watumiaji wa barabara yakiwemo magari ya nchi za nje.

“Nakerwa sana na tabia ya mtu au kikundi ndani ya kijiji kwa kujihusisha na uwekaji wa vizuizi barabara kwa kisingizio cha kushinikiza kiongozi kutatua kero jambo hilo sasa tayari kamati za ulinzi za wilaya na mkoa nimeziagiza kufatilia mwarobaini wa kulikomesha suala hili,”alisema Bendera.

Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wananchi hao kufuata taratibu za kutatua kero ndani ya vijiji kupitia ngazi stahiki ikiwemo kuonana na uongozi wa ngazi ya kitongoji, kijiji, kata, tarafa, wilaya, hadi kufika mkoa na taifa na kuwa njia hizo zikielezwa juu ya kero husika, kero hizo zitapatiwa ufumbuzi.

Bendera alitaja mwarobaini wa kukomesha tabia hiyo kwa wale wataojihusisha na uwekaji wa vizuizi kuanzia sasa ni kuwa ni kukabiliwa na hatua za kisheria zikiwemo kukamatwa na kupelekwa mahakamani na sheria utafuata mkondo wake. HABARI NA MTANDA BLOG.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: