Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja.
WATU
20 wa familia moja akiwamo Ofisa Mtendaji wa kata katika kitongoji cha
Igogo A kata ya Nyampurukano wilayani Sengerema, wamelazwa katika
Hospit
ali Teule ya wilaya hiyo baada ya kula chakula kinachohofiwa kuwa
na sumu.
Watu hao wanadaiwa kula chakula hicho cha usiku Oktoba 23, mwaka huu.
Imeelezwa kwamba mara baada ya kula chakula hicho, walianza kusikia
maumivu makali ya tumbo na kulazimika kukimbizwa hospitalini kwa
uchunguzi na matibabu.
Aidha, baba wa familia hiyo amelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) kutokana na hali yake kuwa mbaya zaidi.
Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Mary Jose, alithibitisha kulazwa
hospitalini hapo kwa watu hao tangu Alhamisi iliyopita kwa hofu ya kula
chakula chenye sumu.
Hata hivyo, Dk. Jose alisema aina ya sumu iyohofiwa kuliwa na watu hao, bado haijafahamika.
''Ni kweli wagonjwa hao wapo lakini haijafahamika chanzo halisi cha
matatizo yao na uchunguzi ulikuwa bado unafanywa kubaini hasa chanzo
chake," alisema Dk. Jose.
Hata hivyo, alisema baadhi ya watu hao wameanza kupata nafuu lakini wengine hali zao bado mbaya.
Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Sofia Manyilizu, alisema serikali kwa
kushirikiana na vyombo vya dola na madaktari, walikuwa wanajaribu
kuchunguza chanzo cha tukio hilo.
''Mimi kama mlinzi wa amani wa kata ya Nyampurukano lilipotokea tukio,
nilifika na kuchukua maelezo ya awali pamoja na orodha, ambapo jumla ya
watu 20 wakiwamo na watoto, wameathiriwa na tukio hilo," alisema.
Miongoni mwa waliothiriwa na chakula hicho ni wazazi, watoto, wajukuu na
vitukuu ambapo baba wa familia hiyo, Stanslaus Kisinza, hali yake bado
ni mbaya.
Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja, ambaye yuko mkoani
Shinyanga kikazi, alitoa pole kwa familia hiyo na kusisitiza kuwa tukio
hilo ni lazima lifanyiwe uchunguzi wa kina.
"Taarifa za tukio hili nimezipata leo (jana), baada ya kuwasili mkoani
hapa (Shinyanga) kikazi nikitokea Dar Salaam na kwa hakika limenishtua
sana," alisema. CHANZO:
NIPASHE
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / CHAKULA CHENYE SUMU CHAWALAZA WATU 20 WA FAMILIA MOJA KATIKA HOSPITALI TEULE YA SENGEREMA.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment