BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DADA WA MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE ANATARAJIWA KUZIKWA KESHO MACHAME.


DADA yake Mwenyekiti wa Taifa Chadema (KUB) Freeman Mbowe anatarajia kuzikwa kesho nyumbani kwao Machame.


Kifo cha dada huyu kilitokea papo hapo baada ya gari alilokuwa akiendesha kupasuka gurudumu la mbele na kuing

ia chini ya daraja baada ya kupinduka na kusababisha watu wawili kupoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa vibaya.
Grace Aikaeli Mbowe, anayesadikiwa kuwa na umri kati ya miaka 47 hadi 50, alikuwa akiendesha gari yenye namba T 277 CAJ aina ya Toyota Cresta akiwa na mumewe aliyefahamika kwa jina la Ibrahim Lukindo (52), wakitokea Jijini Tanga, walipata ajali hiyo eneo la Kabuku wilayani Handeni.

Kamanda wa polisi mkoani Tanga (ACP) Costatine Massawe alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kupitia kwa Ofisa wake wa upelelezi mkoani Tanga,Aziz Kimata, kwamba ajali hiyo ilitokea majira ya saa 1:30 asubuhi Septemba 29/2013  katika eneo hilo baada ya gari hilo kupasuka gurudumu la mbele la kulia kisha kuingia chini ya daraja lililokuwepo eneo hilo.

"Ni kweli kuna ajali ilitokea eneo la Kabuku gari aina ya Cresta lililokuwa likiendeshwa na ndugu inavyosemekana wa Bw Freeman Mbowe, limepata ajali baada ya kupasuka tairi la mbele na kuacha barabara na kuingia chini ya daraja .

"Dereva anayeitwa Grace Aikael Mbowe na mtu anayesemekana ni mumewe anayeitwa Ibrahim Lukindo, wamefariki na watu watatu waliowachukua wamejeruhiwa," alisema RCO Kimata.

Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni pamoja na Bw Ridhiwani Bakari (29) aliyekuwa na mkewe Zeddy Nzuke (29) raia wa Kenya aliyekuwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili na miezi minne aliyefahamika kwa jina la Mariam Ridhiwan ambao kwa sasa wamelazwa katika hospitali ya Magunga wilayani Korogwe.

RCO Kimata aliyezungumza kwa niaba ya kamanda huyo wa polisi alisema chanzo cha ajali hiyo inasemekana kimetokana na kupasuka kwa mpira huo na mwendo kasi wa kawaida na kwamba majeruhi na maiti zi9mehifadhiwa kwenye hospitali hiyo.

Mwandishi wa habari hizi, aliyefika kwenye hospitali hiyo na kuzungumza na Ridhiwani pamja na mkewe ambaye amelazwa wodi namba mbili ya wanawake katika hospitali hiyo, alisema kwamba ndoto zake za kufanya kazi Dar es salaam zimezimika ghafla kutokana na kwamba alikuwa aende kupamba kazi ya uofisa ugavi katika taasisi moja ya fedha ya marehemu Mbowe Jijini Dar es salaam.

"Nilikuwa naenda kupewa kazi na mama Mbowe katika Institution yake ya Micro-Financial Jijini Dar es salaam, mimi ni procurement (Mgavi-manunuzi) na ni Mkenya kwetu ni Eastern Province Kang'undo na nimeolewa na bwana Mtizedi...Lakini sasa ndoto zangu za kufanya kazi Dar es salaam zimezimika ghafla," alisema Zeddy akiwa kitandani amelala na mwanwe ambaye alikuwa haongei tangu amefika katika hospitalini hapo.

Mumewe na mwanamke huyo akizungumzia ajali hiyo alisema kuwa hakuwa akijua kwani alikuwa amelala dakika tatu kabla ya kutokea ajali hiyo ambapo alishtukia yeye, mkewe na mwanawe wametupwa chini kwenye majani wakiwa hawajijui na walikimbizwa katika hospitali hiyo ya Korogwe

Ridhin ambaye ni mkazi wa Nguvumali Jijini Tanga, alisema safari yao hiyo ilikuwa ifanyike Jumamosi mchana lakini kutokana na na kuchelewa kwa wenyeji wao hao, waliondoka Tanga kwenye hoteli ya Doliphin walikolala majira ya saa 11:00 alifajiri kwa ajili ya kwenda Jijini Dar es salaam.

Muuguzi wa zamu wa hospitali hiyo Bi Nayela Missingo alikiri kuwapokea wagonjwa hao ambapo alisema wanafanya jitihada za kuwahamishia katika hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam mtoto Mariam ambaye amepata majeraha katika kichwa chake na kwamba tangu afikishe hospilaini hapo hakuwa katika hali nzuri, haongei walakunyonya.

Bi Zeddy Nzuke na mtoto wake wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Magunga wilayani Korogwe baada ya kupata majeraha katika ajali hiyo.


CHANZO.
Noel Olevaroya
Noel Olevaroya
Dada yake M/kiti wetu wa Taifa Chadema (KUB) F.Mbowe anazikwa kesho nyumbani kwao Machame,habari ziwafikie makamanda wote wa Chadema,Tulimpenda sana lkn Mungu kampenda zaidi.
Like · · · about an hour ago near Arusha, Dar es Salaam ·
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: