BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HIKI NDICHO CHANZO CHA KUFARIKI DUNIA KWA MTANGAZAJI MKONGWE JULIUS NYAISANGAH 'UNGLE J'.

JULIUS NYAISANGA (KATIKATI).

MOROGORO/DAR ES SALAAM.
MTANGAZAJI mkongwe nchini, Julius Nyaisanga ‘Uncle J’ (53), alifariki dunia jana mkoani Morogoro baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kisukari na moyo.
Meneja wa Matangazo wa Kituo cha Abood Media ya Morogoro, Abeid Dogoli alisema Nyaisanga alifariki dunia jana saa moja asubuhi katika Hosp
itali ya Mazimbu, Manispaa ya Morogoro alikokuwa amelazwa.
Nyaisanga alikuwa miongoni mwa wakuu wa idara katika Kituo cha Televisheni cha Abood Media.
Dogoli alisema kuwa taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Kihonda na kwamba wanatarajia kumsafirisha kwenda nyumbani kwao mkoani Mara kwa maziko ingawa taarifa zaidi zitatolewa kama kutakuwa na mabadiliko.
Akizungumzia kifo hicho, mke wa mtangazaji huyo, Leah Nyaisanga alisema hali ya mumewe ilibadilika ghafla kwa kuzidiwa ambapo juzi aliwahishwa katika Hospitali ya Mazimbu ambako alifikwa na mauti.
Marehemu Nyaisanga ameacha watoto watatu ambao ni  Samuel, Noela na Beatrice.
Naye Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Aziz Abood ambaye familia yake ndio wamiliki wa Kituo cha Abood Media, alisema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa msiba huo wa meneja huyo aliyekuwa mchapakazi.
Nyaisanga aling’ara Radio Tanzania
Dar es Salaam (RTD) na Redio One.
Nyaisanga ni kati ya watangazaji waliong’arisha tasnia ya utangazaji nchini Tanzania na hata nje ya nchi.
Alianzia kazi RTD, pia aliwahi kufanya kazi katika Kampuni ya IPP akiwa kama mtangazaji na baadaye Mkurugenzi wa Radio One.
Pia alifanya kazi na Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle), Sauti ya America, Redio Japan na Ghana. MWANANCHI.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: