abili katika mahakama ya hakimu mkazi Morogoro jana.
PICHA/JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
PICHA/JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
PICHA/JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Waumini wa dini ya kiislamu wakiwa wamekunja ngumi huku wakitamka maneno ya kiaraba "Taqri allah Akiball yakiwa na maana ya mungu mkubwa" wakati wakielekea katika msikiti mkuu wa mkoa wa Morogoro kupata maelezo ya Sheikhe Ponda kutokana na baadhi yao kushindwa kusikiliza kesi hiyo, hapa ni barabara ya zaamani ya Dar es Salaam eneo la Lotto wakitokea mahakama ya hakimu mkazi Morogoro. PICHA/JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
PICHA/JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Ombi la kufutiwa shitaka moja liliwakilishwa na Wakili wa Sheikh Ponda, Juma Nassoro, mahakamani hapo Septemba 17, mwaka huu, akitaka shitaka la kwanza la kutotii amri halali linalomkabili mteja wake lifutwe.
Wakili Nassoro alidai kuwa mahakama hiyo haina uwezo kisheria kusikiliza shitaka hilo, vinginevyo lifunguliwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Kesi hiyo imeahiriswa mpaka Novemba 7 mwaka huu ambapo mahakama itaanza kusikiliza mashahidi wa kesi hiyo. Sheikh Ponda amerudiswa rumande.
Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Morogoro leo imetupilia mbali ombi la kufutiwa shitaka moja kati ya matatu yanayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda.
Ponda anakabiliwa na mashitaka matatu; ambayo ni kutokutii amri halali, kuharibu imani za dini na kushawishi kutenda kosa.
0 comments:
Post a Comment