HATUA ya mwisho ya michuano ya kufuzu kombe la dunia kwa Bara la Afrika imeanza hii leo kwenye viwanja viwili tofauti .
Nchini Ivory Coast The Elephants ambao ni timu ya taifa ya Ivory
Coast waliwakarib
isha Senegal katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa
taifa wa nchi hiyo.
Ivory Coast wakiongozwa na Didier Drogba walishinda mchezo kwa
matokeo ya 3-1 baada ya mabao ya Drogba , Salomon Kalou huku bao lingine
likiwa la kujifunga mwenyewe toka kwa mlinzi wa Senegal Ludovic Sane.
Mwishoni kabisa mwa mchezo huo Senegal walipata la ugenini ambalo
linawapa matumaini kwenye mchezo wa marudiano ambalo lilifungwa na
mshambuliaji Papiss Demba Cisse.
Matokeo haya yanawafanya Ivory Coast kwenda kwenye mchezo wa
marudiano wakiwa na matumaini ya kusonga mbele huku wakifahamu kuwa
wanahitaji kupata walau sare ili kukata tiketi ya kwenda Brazil.
Kwingineko Burkina Faso wakiwa kwenye uwanja wao wa Agosti 4
waliwafunga Algeria 3-2 katika mchezo uliokuwa na upinzani wa aina yake.
Mabao ya Burkinabe yalifungwa na Jonathan Pitroipa , Aristide Bance
na Djakaridja Kone huku Algeria wakifunga kupitia kwa Soufiane Feghouli
na Carl Medjani.
Michezo hii itaendelea hapo leo wakati ambapo Nigeria watacheza na
Ethiopia huko Addis Ababa huku Tunisia nao wakicheza na Cameroon.
Siku
ya jumanne Ghana watakuwa wenyeji wa Misri .
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / IVORY COAST YAJILILIA NIA YA BRAZIL KWA KUINYUKA SENEGAL 3-1 HUKU BURKINA FASO WAKIITANDIKA ALGERIA 3-2 KATIKA MBIO ZA KUWANIA KUFUNZO KOMBE LA DUNIA KWA UKANDA WA AFRIKA.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment