Nassor Masoud 'Cholo', akimtuliza Hamis Ally wa Prison wakati alipokuwa akivuta mpira kuelekea golini kwa timu hiyo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo huo Simba ilishinda kwa bao 1-0.
JIJI Dar es salaam uwanja taifa uliwashuhudia vinara wa ligi hiyo Simba Sports Club wakiendeleza mwanzo mzuri wa ligi hii baada ya kuwafunga Tanzania Prisons kwa bao moja bila .
Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na kiungo Jonas Gerard Mkude kwa shuti la nje kidogo ya eneo la kumi na nane .
Huko Kaitaba mjini Bukoba Dar es salaam Young Africans waliwafunga wenyeji wao Kagera Sugar kwa mabao mawili kwa moja .
Mabao ya Yanga yalifungwa na Hamis Kiiza na Mrisho Ngassa.
Simba wanaendelea kuongoza ligi kuu ya Tanzania wakiwa na pointi 18 huku Yanga wakiwa na pointi 15.
0 comments:
Post a Comment