BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KAMERA ZA CCTV ZAFICHUA SIRI YA MAGAIDI WA KUNDI LA KIISLAM LA AL-SHABAAB KATIKA UVAMIZI WA JUMBA LA MADUKA YA WESTGATE MALL NA KUWAPIGA RISASI RAIA WASIO NA HATIA MJINI NAIROBI KENYA.

Nairobi. Picha zilizonaswa kupitia kamera za CCTV zilizofungwa kwenye jengo la kibiashara la Westgate Mall mjini Nairobi zinaonyesha kwamba magaidi waliov
amia jengo hilo walikuwa wanne, hivyo kuanza kuibua mtizamo mpya kuhusu magaidi waliovamia jengo hilo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, taarifa hizo ambazo bado si rasmi kutoka kwa mmoja wa maofisa wa juu wa Serikali ya Kenya juzi, zilieleza kwamba watu wanne wakiwa na silaha za kisasa ndio walioonekana kupitia kamera hizo za siri, hivyo kuanza kuwepo kwa uwezekano wa kupungua kwa idadi ya awali ya watuhumiwa hao wa ugaidi waliovamia jengo hilo.

Awali, Serikali ya Kenya ilieleza kwamba wavamizi hao ambao walijitambulisha kuwa wafuasi wa kundi la kigaidi la Al Shabaab la Somalia waliotekeleza uvamizi huo Septemba 21, walikuwa kati ya 10 hadi 15 na kusababisha vifo vya watu 67, idadi ambayo imeanza kutiliwa walakini.

Kati ya waliouawa, kwa mujibu wa taarifa za Serikali, walikuwemo wanausalama sita, watatu wakiwa maofisa usalama wa jeshi na watatu wakiwa maofisa usalama wa polisi ambao waliuawa kwati wa kujibizana risasi walipokuwa wakijaribu kuwadhibiti wavamizi hao.

Taarifa hizi zimeanza kuvuja wakati wataalamu wa masalia ya miili ya binadamu wakiendelea kufanya uchunguzi kwenye mabaki ya miili ya watu waliokuwa wamenasa kwenye vifusi vya jengo hilo.

Wakati uchunguzi huo ukiendelea, tayari vijana kadhaa wameshakamatwa kwenye eneo la watu wa makazi duni la majengo mjini Nairobi, kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano kama sehemu ya polisi kujaribu kuwanasa wavamizi hao ambao kwa mujibu wa taarifa za awali, walifanikiwa kutoroka kupitia mtaro wa maji machafu unaotoka kwenye jengo hilo.


HII NI VIDEO IKIONYESHA PICHA ZA KAMERA YA CCTV NDANI YA JENGO LA WESTGATE MALL..
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: