KISA CHA MKUU WA KITUO CHA POLISI KILINDI EDWARD LUSEKELO KUJERUHIWA KWA RISASI CHABAINIKA MKOANI TANGA.
Na Oscar Assenga,Kilindi.
MGAMBO wa Kijiji cha Lwande Wilayani hapa, Salum Mgonje amekufa kwa kushambuliwa na mapanga na kundi la watuwaliokuwa wakipinga kitendo cha mwenzao kulipishwa ushuru wa manunuzi ya zao la hiliki wa Serik
ali ya Kijiji.
Mashambulizi hayo baadaye yalizusha mapigano baina ya kundi la watu waliokuwa wakimsaidia mfanyabiashara huyo na askari wa jeshi la polisi walipokwenda kuwakamata waliohusika na mauaji ya mgambo.
Katika mapigano hayo, Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kilindi Edward Lusekelo, ambaye aliongoza askari waliokwenda kuwakamata wahusika na mauaji ya Mgambo alijeruhiwa kwa kupigwa risasi kwa bunduki ya ShortGun.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamnada wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,Constantine Massawe, zilithibitisha kuwa askari wa mgambo mmoja aliuawa juzi mchana katika tukio hilo lililotokea katika kijiji cha Lwande, huku Mkuu wa kituo akijeruhiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Selemani Liwowa alisema chanzo cha mapigano hayo ni mfanyabiashara huyo kutoka Kijiji cha Lulago Kata ya Lwande kwenda Kijiji cha Lwande kununua hiliki ambapo baada ya kukaidi kulipa ushuru mgambo alilazimika kumtia msukosuko ili aweze kulipa kama ilivyo sheria ya kijiji.
Ndiyo chanzo cha kutokea kwa vurugu hizo baina mgambo na wafanyabiashara ambapo baadaye walimshambulia kwa mapanga na kisha kumuua.
Aidha, alisema taarifa za mauaji ya mgambo zilizpofika kituo cha Polisi ilimlazimu mkuu wa kituo kuongoza kikosi kilichokwenda kijiji cha Lwande kwa ajili ya kuwasaka waliohusika na baada ya kuwasili kijijini hapo likajitokeza kundi la watu wenye silaha na kuanza kuwashambulia askari hao jambo lililosababisha askari hao kujibu mashambulizi.
Akithibitisha habari hizi,Kamanda Massawe alisema tayari watu wanne wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa kuhusika na tukio hilo huku mkuu wa kituo cha Polisi akiwa amekimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo kwa ajili matibabu
0 comments:
Post a Comment