BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RUSHWA KUIANGUSHA CCM KATIKA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2015.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wanachama wa chama hicho kwenye moja ya mikutano, Kilosa mjini mkoani Morogoro. Picha ya Maktaba.
 
DODMA.
MWENYEKITI wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete amesema kama rushwa haitakomeshwa ndani ya chama hicho, katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2015 kitaanguka vibaya na iwapo kitanusurika hakitap
ita kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amempa jukumu la kushughulikia viongozi wa CCM wanaokula rushwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philipo Mangula.
Rais Kikwete, alitoa onyo hilo juzi usiku, alipokuwa akifunga mafunzo maalumu ya siku nne kwa makatibu wa mikoa, makatibu na wenyeviti wa wilaya wa chama hicho nchini.
“Kama hatutabadilika katika suala la rushwa mwaka 2015 tutakuwa na wakati mgumu sana na kama mwaka huo tutafanikiwa kuishika Serikali, basi mwaka 2020 hatutarudi tena madarakani.
“Najua rushwa ipo na mnaendelea kupokea shilingi laki mbili za airtime (muda wa mawasiliano), ndugu zangu hatutafika ama wengine watavuka na wengine kukwama,” alisema Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete.
Hii ni kauli ya kwanza nzito ya Rais Kikwete ya hivi karibuni ya kukionya chama hicho kuhusu uimara wake wa kuendelea kushika dola.
Aliendelea kusema kuwa tatizo la rushwa kwa viongozi wa chama hicho linazidi kuwa kubwa kila siku, hali ambayo inawapotezea imani wananchi ambao ndio wapiga kura wao.
“Viongozi wa chama ndio mmekuwa mawakala wa kusambaza rushwa bila hata aibu. Nawaombeni tubadilike, kama tutaendelea hivi hali yetu itakuwa ngumu sana katika chaguzi mbalimbali, nawaambieni,” alisema Rais Kikwete ambaye alitumia muda wa saa mbili kufunga mafunzo hayo.
Aliwaambia kuwa siku hizi watu wana mbadala wa vyama vingine na siyo CCM peke yao.
Aidha, Rais Kikwete alisema viongozi ambao wanajihusisha na vitendo vya rushwa waondolewe mara moja katika nafasi zao, ili kuwaweka watu watakaokisaidia chama kupata mafanikio.
“Tuna vijana wengi kutoka katika vyuo mbalimbali ambao wanaweza kufanya kazi kwa uadilifu wa hali ya juu, hivyo hatuna budi kuachana na hawa wala rushwa ambao watatupotezea sifa yetu kwa wananchi.
“Tukipoteza urais ndiyo tumekwisha na chama kinaweza kufa.” MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: