BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

LICHA YA TANZANIA KUWA NCHI YENYE AMANI NA UTULIVU LAKINI WANANCHI WAKE NI MIONGONI MWA WATU WASIO NA FURAHA NA WALIOKATA TAMAA YA MAISHA.

 
mwanamke huyu akiwa amepewa msaada na wasamaria wema ili kumwahisha hospitali UMASIKINI nijanga lisilo kubalika katika jamii yoyote.

DAR ES SALAAM.
TANZANIA ikitajwa kuwa ni miongoni mwa nchi zenye amani na utulivu, imebainika kuwa Watanz
ania ni miongoni mwa watu wasio na furaha na waliokata tamaa hapa duniani.

Ripoti inayoonyesha orodha ya nchi zenye furaha duniani ya mwaka 2013 (World Happiness Report 2013), imeitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi 10 za mwisho duniani kati ya nchi 156 zilizofanyiwa utafiti huo.President Jakaya Kikwete.

Ripoti hiyo iliyoandaliwa na kundi la wataalamu kutoka Umoja wa Mataifa (UN), kati ya mwaka 2010 na 2012, inaonyesha kuwa Tanzania imeshika nafasi ya 151 ikiburuta mkia pamoja na nchi za Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Benin na Togo.

Upatikanaji wa huduma za jamii, mtazamo wa watu kuhusu rushwa, umri wa kuishi, ukosefu wa kazi, pato la taifa na ukarimu wa watu katika nchi husika, ni baadhi ya vigezo vilivyoangaliwa wakati wa kuandaa taarifa hiyo.

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka alieleza kushtushwa na ripoti hiyo kwa maelezo kwamba ni asilimia 11.7 tu ya Watanzania wasio na ajira na kwamba wale wanaofanya kazi, wanapata huduma zote za msingi, ikiwa ni pamoja na kwenda likizo na mishahara inayolingana na taaluma zao.ZAHANATI zinahitajika vijijini nchini tanzania kote zinawe jutoa huduma bora wauguzi wakutosha maabara bora na zenye vifaa vya kisasa magari ya wagonjwa LAKINI NCHINI TANZANIA usishangae viongozi kujipongeza kwakupata nyadhifa wakiishi maisha ya kifahari huku watu wakifa kwakukosa dawa mahospitalini wajawazito wakifia njiani kutokana na ubali wa kituo cha afya shule zikiwa hazina vyooo walimu hawapo wakutosha majengo mabovu madawati hakuna vitabu hakuna na kila kanda na mtaala wake  AMAKWELI KUFA KUFAANA TANZANIA viongozi matajiri wananchi masikini wakutisha UMASIKINI WA TANZANIA janga la kupandikizwa NITAUCHUKIA UMASIKINI NA KUUPIGA VITA HADI TONE LA MWISHO LA DAMU YANGU nakataa umasikini ujinga na maradhi sio haki ya watanzania

“Watanzania wana furaha, kwa upande wa wafanyakazi wanapata haki zao zote wanazostahili, sijui ni vigezo vipi wametumia…kwa mujibu wa takwimu za 2006 ni asilimia 11.7 ya Watanzania ndio waliokuwa hawana kazi, lakini wakati huo idadi ya watu ilikuwa ndogo, hivi sasa imeongezeka,” alisema Kabaka na kuongeza:“Usafiri ndiyo tatizo linalowasumbua wafanyakazi wengi kwa kuwa wanachelewa kwenda kazini.”

Naye, Naibu Waziri wa Fedha, Saada Salum alisema pamoja na vigezo vingine vilivyotumika kutambua furaha ya Watanzania, umaskini ndiyo unaoweza kuwa chanzo cha Tanzania kushika nafasi za mwisho.

“Inategemea na vigezo vingine walivyovitumia, nakubali kuwa Tanzania ni maskini pengine hali hiyo imeifanya nchi kushika nafasi ya mwisho,” alisema Salum.

Nchi zilizoongoza

Taarifa hiyo imezitaja nchi tano; Denmark, Norway, Uswisi, Netherlands na Sweden kuwa ndizo zinazoongoza kwa watu wake kuwa na furaha zaidi duniani, huku Angola ikishika nafasi ya kwanza Afrika na ya 61 duniani ikifuatiwa na Algeria (73), Libya (78), Ghana (86), Zambia (91), Lesotho (98), Morocco (99) na Swaziland (100).

Kwa upande wa Afrika Mashariki, wananchi wa Uganda ndio walionekana kuwa na furaha zaidi kwani nchi hiyo imeshika nafasi ya 120 wakifuatiwa na Kenya (123), Tanzania (151), Rwanda (152) na Burundi (153).

Ripoti hiyo inabainisha kuwa kati ya mwaka 2005 na 2012, nchi 60 duniani ziliongeza viwango vya furaha kwa watu wake, kati ya hizo 16 zikiwa barani Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: