Hadija Nyembo.
MAHAKAMA ya Wilaya ya Chato mkoani Geita imeamuru kukamatwa kwa aliyekuwa Mkuu
wa wilaya hiyo, Hadija Nyembo na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya
wilaya hiyo, Hamida Kwikwega, kuunganishw
a kwenye kesi ya ubadhilifu wa
pembejeo za kilimo.
Hatua hiyo imekuja baada ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia
Rushwa(Takukuru) wilayani hapa, kuiomba mahakama hiyo kutoa hati maalumu
ya kuwakamata watuhumiwa hao ili wafikishwe mahakamani kujibu tuhuma
zinazowakabili.
Mwingine anayetakiwa kukamatwa ni aliyekuwa Ofisa kilimo na Mifugo wa wilaya hiyo, Dk. Phares Tongola.
Takukuru imewafikisha watuhumiwa wengine ambao ni namba 4 na 5 katika
kesi hiyo na nyadhifa zao kwenye mabano, Mery David, (Wakala wa
Usambazaji wa pembejeo za kilimo kata ya Buseresere), na Mageni Mbassa
(Kaimu mtendaji wa kijiji cha Mapinduzi) wilayani hapa.
Watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 63 yenye makosa matano,
yakiwamo ya kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri, kutumia
madaraka vibaya, ubadhilifu wa fedha za umma, kusaidia kutenda kosa na
kughushi nyaraka.
Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Chato, Jovith Katto, aliamuru
washitakiwa hao kwenda mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya
dhamana.
Wakati mashtaka hayo yakisomwa mahakamani, mshitakiwa namba moja
aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato (Nyembo), ambaye kwa sasa ni Mkuu wa
Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, namba mbili aliyekuwa Mkurugenzi wa
halmashauri hiyo (Kwikwega), na namba tatu, Ofisa kilimo wa wilaya hiyo
Dk, Tongola, hawakuwapo mahakamani.
Mwendesha mashitaka wa Takukuru, Kelvin Murusuri, alisema watuhumiwa hao
walitenda makosa hayo kati ya Oktoba 10, 2010 hadi Januari mosi, 2011,
ambapo kwa pamoja walisababisha hasara ya mamilioni ya fedha za
serikali.
Murusuri aliiomba mahakama hiyo kutoa hati maalumu ya kuwakamatwa
watuhumiwa wengine ambao hawakuwapo mahakamani ambao ni namba moja hadi
tatu ili waunganishwe na wenzao, ombi lililokubaliwa na mahakama hiyo.
Hakimu Katto alisema mahakama hiyo imekubali kutoa hati ya kuwakamata
watuhumiwa wengine na kwamba kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 25, mwaka
huu. CHANZO:
NIPASHE
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / MAHAKAMA YA WILAYA CHA CHATO YATOA YAAMURU KUKAMATWA KWA ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA HIYO, HADIJA NYEMBO KWA TUHUMA ZA UBADHILIFU WA PEMBEJEO ZA KILIMO.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment