WANAMGAMBO wa al-Shabab wamedhibiti hali katika mji
wa Barawe, ambako makomando wa Marek
ani walijaribu kumkamata mmoja wa
viongozi wa kundi hilo mnamo Jumamosi.Inaarifiwa kuwa operesheni ya makomando hao ilikuwa inamlenga raia mmoja msomali kwa jina Abdikadir Mohamed Abdikadir akijulikana kwa jina lengine kama Ikrima.
Operesheni hiyo inafanyika baada ya shambulizi la kigaidi nchini Kenya mwezi jana.
Al-Shabab, ambayo ni tawi la al-Qaeda, imekiri kutekeleza shambulizi hilo ambalo lilisababisha vifo vya watu 67.
Hata hivyo maafisa wa eneo hilo bado hawajathibitisha ambako operesheni hiyo ya jumamosi iliyotibuka ilikofanyika
Siku hiyo hiyo majeshi ya Marekani yalimkamata kiongozi wa Al al-Qaeda Anas al-Liby mjini Tripoli.
Anashukiwa kuongoza mashambulizi ya kigaidi dhidi ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998.
Wenyeji wanasema kuwa Ikrima ni mmoja wa viongozi wa al-Shabab akiwa na jukumu la kupanga mikakati ya kundi hilo na kuwa huwa amezingirwa na walinzi 20 walio na silaha nzito.
Mapema Jumamosi, wanajeshi wa Marekani waliwasili katika nyumba yake karibu na bahari hindi ambako Ikrima hukaa mara kwa mara.
Walipokuwa wanaweka ngazi nje ya nyumba, mlinzi alitoa kilio kuhusu watu kuingia katika eneo hilo na kusababisha ufyatulianaji wa risasi uliodumu kwa dakika 20.
Al-Shabab imesema kuwa mmoja wa wapiganaji wake aliuawa wakati wa ukabilianaji huo wa risasi.
Mwandishi wa BBC Mohammed Moalimu anasema kuwa wenyeji sasa wanahofia kutumia simu zao wasije wakadaiwa kuwa wapelelezi wa Marekani.
Al-Shabab imekuwa ikidhibiti eneo hilo tangu mwaka 2008.
Walipoulizwa ikiwa serikali ilifahamu kuhusu uvamizi huo, serikali ilisema kuwa ushirikiano wao na washirika wao wa kimataifa kupambana na ugaidi sio siri.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry alisema kuwa harakati dhidi ya ugaidi nchini Libya na Somalia zilionyesha kuwa Marekani kamwe haitachoka kuwachukulia hatua wanaofanya vitendo vya kigaidi.
Al-Shabab wamelazimia kutoroka miji mikubwa nchini Somalia kwa miaka miwili iliyopita kufuatia operesheni za jeshi la Muungano wa Afrika ingawa bado linadhibiti maeneo mengi ye mashinani.
CHANZO SHIRIKA LA HABARI LA BBC.
0 comments:
Post a Comment