BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAREKANI YAFUNGUA MASHTAKA MAPYA DHIDI YA WALINZI WA KAMPUNI YA ULINZI YA BLACKWATER KWA MAUAJI YA RAIA 14 NCHINI MAGHDAD MWAKA 2007.

** FILE ** In a file photo Plainclothes contractors working for Blackwater USA take part in a firefight as Iraqi demonstrators loyal to Muqtada Al Sadr attempt to advance on a facility being defended by U.S. and Spanish soldiers, Sunday, April 4, 2004 in the Iraqi city of Najaf, The State Department may phase out or limit the use of private security guards in Iraq, which could mean canceling Blackwater USA's contract or awarding it to another company in line with an Iraqi government demand, The Associated Press has learned. (AP Photo/Gervasio Sanchez)e Mlinzi wa kampuni ya Blackwater.

MAREKANI imewafungulia mashtaka mapya ya kuua bila kukusudia walinzi wa kampuni ya ulinzi ya Blackw
ater Worldwide kwa mauaji ya mwaka 2007 mjini Baghdad nchini Iraq 


Waendesha mashtaka wanasema raia 14 ambao hawakuwa na silaha waliuwawa kwenye mauaji hayo, ambapo walinzi waliwamiminia risasi Wairaki. 

Mauaji hayo yalisababisha msuguano katika uhusiano kati ya Marekani na Irak na kuongeza wasiwasi juu ya hatu ya Marekani kutumia walinzi wa kampuni binafsi za usalama, ambao walikuwa na kinga dhidi ya kushtakiwa nchini Iraq.

Mashtaka ya kwanza ya Marekani yaliyowasilishwa dhidi ya walinzi wa kampuni ya Blackwater mnamo mwaka 2008, yalitupiliwa mbali mwezi Desemba mwaka 2009, yapata mwezi mmoja kabla tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo. Jaji wa mahakama moja ya Marekani alipitisha kwamba waendesha mashtaka walitakiwa kufanya mengi zaidi kuacha nje kauli walizozitoa walinzi hao wakiwa chini ya kitisho cha kupoteza ajira zao.

Kesi hiyo ilianzishwa tena mwaka 2011 na waendesha mashtaka wakaanza tathmini ndefu ya mashtaka ambayo wangeweza kuyathibitisha mahakamani. Kesi hii mpya inajumuisha mashtaka 33, yakiwemo mauaji bila kukusudia, jaribio la kuua bila kukusudia na kutumia silaha katika uhalifu wa kutumia nguvu. Walinzi wamesema hawana hatia kwa mashtaka hayo yanayofanana na yale yaliyowasilishwa dhidi yao miaka mitano iliyopita.

Majina ya walinzi hao ni - Paul Slough mwenye umri wa miaka 34, Nicholas Slatten; 29, Evan Liberty, 31; na Dustin Heard, 32. "Tumevunjika moyo kwamba wizara ya sheria imeamua kuendelea na kesi hii, ambayo tunaamini haina msingi wowote kabisa," amesema Dave Schertler, wakili wa Heard, katika taarifa yake.

Ni mauaji yasiyo halali
Waendesha mashtaka wamesema wanaume hao walitumia bunduki za kulenga shabaha, bunduki za rashasha na maguruneti wakati wa shambulizi la ufyetuliaji risasi katika uwanja wa Nisur mjini Baghdad, ambapo watu 14 waliuwawa na wengine 18 kujeruhiwa.
A armed man working for a private security company sits on the back of a vehicle in Tahrir Square, central Baghdad, Iraq, on Monday, Oct. 8, 2007. An official Iraqi investigation into the Blackwater shootings on Sept.16, in Baghdad, has raised the number of Iraqis killed to 17 six more than previously thought and concluded the gunfire was not warranted and that those involved should face trial.(AP Photo/Hadi Mizban) Gari la Blackwater mjini Bagdad.
 
"Wakala nyingi za Marekani zilizohudumu nchini Iraq zilifanya hivyo kwa heshima na taadhima, lakini kama inavyotuhumiwa leo, watetezi hawa walitumia vibaya mamlaka yao kupitia shambulizi la kiholela dhidi ya raia ambao hawakuwa na silaha, shambulizi ambalo lilipitiliza uwezekano wa kuhalishwa," amesema wakili wa Marekani, Ron Machen, ambaye ni mwendesha mashtaka mkuu mjini Washington, katika taarifa yake.

Kumepangwa kufanyika kikao maalumu cha mahakama kuhusu kesi hiyo inayowakabili walinzi hao wa kampuni ya Blackwater Ijumaa wiki ijayo. Tarehe ya kusikilizwa kesi hiyo haijawekwa na wakili wao alisema kwenye kikao cha mwezi uliopita kwamba huenda ikachukua miaka kadhaa kabla kesi hiyo kuanza.

Mwezi uliopita waendesha mashtaka walifutilia mbali mashtaka dhidi ya mlinzi wa tano wa kampuni hiyo, Donald Ball, wakisema wametumia mamlaka waliyo nayo kuzingatia tathmini ya ushahidi uliopo dhidi yake. Kampuni hiyo ya Blackwater ilibadili jina na sasa inajulikana kama Academi na makao yake yako McLean katika jimbo la Virginia. DW
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: