MBUNGE WA MORO MJINI ASHTUKIA UFISADI KATIKA UJENZI WA MADARAJA NA KUTISHIA KUISHTAKIA MANISPAA KATIKA KAMATI YA BUNGE YA MAHESABU YA SERIKALI ZA MITAA.
Hili ndilo daraja jipya la mto Mzinga linalojengwa na fundi ujenzi Dany Samwel ambalo linadaiwa kujengwa chini ya kiwango likitenganisha kijiji cha Mlulu na Kilala kata ya Luhungo Manispaa ya Morogoro kwa tham
ani sh13.9 milioni mkoani, Jambo ambalo mbunge wa jimbo la Morogoro mjini amelipinga na kutaka wahusika kumsaka fundi huyo kurudia ujenzi huo kwa kiwango kinachokubali vingine arudishe pesa ama la sivyo yupo tayari kuishtakia Manispaa katika kamati ya mahesabu ya bunge. PHOTO/MTANDA BLOG
Mhe Mbunge wa jimbo hilo akitembea kwa tahadhari katika mwamba wa jiwe kuelekea katika daraja lingine ambalo lilijengwa na fundi ujenzi. PHOTO/MTANDA BLOG
Hili ni daraja lingine la mto Kilala ambalo tayari ujenzi wake umekamilika. PHOTO/MTANDA BLOG
Akisaini kitabu cha wageni katika kijiji hicho.
Akisiliza taarifa fupu kabla ya kuanza kazi ya ukaguzi wa madaraja hayo.
Na Juma Mtanda, Morogoro.
MBUNGE wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood ametishia kuishtakia halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa Kamati ya kudumu ya bunge ya mahesabu za serikali za mitaa kutokana na watalaam wake kushindwa kusimamia vyema miradi ya ujenzi wa madaraja ya waenda kwa miguu katika mito ya Mzinga na Kilala iliyoghalimu kiasi cha sh sh13.9 milioni ikidaiwa kujengwa chini ya viwango kata ya Luhungo Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na wananchi kwa tofauti wakati wa ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa madaraja hayo katika kata hiyo katika mitaa ya Kilala na Mlulu, Abood alisema kuwa amesikitishwa kuona viwango vibovu vya ujenzi wa madaraja hayo hali ambayo anadaiwa imechangiwa na ofisi ya mkandalasi upande wa barabara kushindwa kusimamia ujenzi huo na kusababisha upotevu wa fedha za wananchi kutumika vibaya jambo ambalo linarudisha nyumba maendeleo ya wananchi wa kata hiyo na taifa kwa ujumla.
Kuna mambo mawili ofisi ya mkandasi Manispaa ya Morogoro wanaweza kufanya juu ya ujenzi ya madaraja hayo kuwa chini ya viwango ikiwemo kumtaka fundi aliyejengwa madaraja hayo kurudisha fedha ama kurudia ujenzi upya vinginevyo yupo tayari kuistkakia halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa kamati ya kudumu ya bunge ya mahesabu za serikali za mitaa. Alisema Abood.
Abood alisema kuwa ana shaka na mchakato mzima wa kumpata mkandalasi wa ujenzi huo na kushangwazwa kupewa kazi mtu binafsi badala ya kampuni inayotambulika.
Abood alisema kuwa madaraja yaliyojengwa katika mito hiyo yamejengwa chini ya kiwango na hali hiyo imetokana na kazi ya ujenzi huo kupewa mtu binafsi badala ya mkandalazi anayetambuliwa jambo anadai limechangia kujengwa madaraja kuwa viwango.
“Nina mashaka na mchakato mzima wa tenda ya upatiakanaji wa ujenzi wa miradi ya madaraja ya mto Mzinga na Mlulu kupewa mtu binafsi badala ya mkandalasi ama kampuni jambo ambalo sasa hivi ndiyo adhali zake zinaonekana wazi wazi hivyo ofisi ya mkandalasi Manispaa ipo haja ya kumsaka aliyengwa arudie kujenga ama arudishe fedha za wananchi ili malengo yao yawe yametimia ya kuondoa kero hiyo”. Alisema Abood.
Abood alisema kuwa kero kubwa wanayokabiliana nayo wananchi wa kata hiyo ya Luhungo pamoja na wanafunzi hasa kipindi cha mvua za masika, mito hiyo kujaa maji kwa kipindi kirefu na wananchi kushindwa kuvuka sehemu moja kwenda nyingine.
Abood alisema kuwa kama mwakilishi wa wananchi katika jimbo la Morogoro mjini katika kuwatetea na kufikisha malalamiko mbalimbali ndani ya Manispaa na bungeni ipo haja kwa halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kufuatilia kwa kina miradi ya ujenzi wa madaraja hayo kujengwa chini ya kiwango huku ikionyesha kazi hiyo kupewa mtu binafsi badala ya mkandalasi.
Naye Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Erick Pearson alisema kuwa makubaliano ya ujenzi wa daraja la waenda kwa miguu yalifanyika desemba 13 mwaka 2010 kati ya kamati ya ujenzi wa madaraja na fundi Daniel Ndaga kwa ghalama za sh13,975,000 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja ya Mzinga na Mlulu.
Pearson alisema kuwa mchakato wa ujenzi wa madaraja hayo kamati hiyo haikushirikisha watalaam kutoka Manispaa ulifanyika kwenye kata na mpaka sasa fundi huyo tayari amelipwa sh12,427,780 milioni na kuahidiwa kulipwa kiasi cha sh1,547,210 milioni kikitarajiwa kulipwa mara baada ya kumalizika kwa kazi hiyo.
0 comments:
Post a Comment