KISA CHA MSAFARA WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, DKT NCHIMBI KUPIGWA MAWE MJINI SONGEA NI KUSHINDWA KUTATULIWA KWA KERO YA DARAJA LA MATARAWE.
Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Dkt Emmanuel Nchimbi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini
Na Stephano Mango,Songea.
MSAFARA wa Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Dkt Emmanuel Nchimbi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma wapig
wa mawe na wananchi waliojitokeza kuzungumzia kero ya daraja la Matarawe ambalo linadaiwa kusababisha vifo vya watu zaidi ya watatu katika mwezi huu wa octoba mwaka huu
Wananchi hao wa kata ya Matarawe Manispaa ya Songea,wakiwemo waendesha Pikikipiki maarufu kwa jina la Yebo Yebo walifunga barabara kwa zaidi ya masaa mawili na kufanya fujo za kung’oa kingo za daraja pamoja na kuweka magogo na mawe katikati ya daraja na kuchoma matairi moto ili Mbunge huyo asipite mpaka atoe majibu ya kina kuhusu daraja
Hali hiyo ililazimisha Jeshi la polisi kuwatawanya wananchi hao kwa kuwafyatulia mabomu ya machozi kwa lengo la kuzuia uharibifu zaidi na kuufanya msafara upite wakati ukirudi kutoka kwenye Mkutano wa hadhara wa Matarawe baada ya kuzuiriwa wakati wa kwenda na wakati wa kurudi ambapo hadi sasa watu nane wanashikiliwa na Jeshi hilo kutokana na vurugu hizo.
Tukio hilo limetokea jana kati ya saa kumi hadi saa kumi na mbili jioni ambapo wananchi hao wakiwa na hasira walifanya fujo hizo wakiwa na lengo la kumshinikiza Mbunge wa Jimbo la Songea mjini ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi awasaidie kupanua daraja la mto Matarawe ambalo ni dogo kwani kwa muda mrefu limekuwa likisababisha ajalli mara kwa mara katika eneo hilo kutokana na ufinyu wa daraja hilo.
Awali Mbunge huyo akiwa katika ziara yake ya siku ya pili akitokea mtaa wa Liumbu kata ya Mletele kukagua shughuli mbali mbali za maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi akiwa anaelekea kata ya matarawe kwenye mkutano wa hadhara ndipo alikutana na umati mkubwa wa wananchi wakiwemo waendesha piki piki walikuwa wamezuia njia na kusimama njiani ili asikilize kero zao kutokana na watu kufa mara kwa mara ambapo siku moja kabla ya mbunge huyo kufanya ziara kuna kijana aliyetambulika kwa jina la Mashaka Nuhu mkazi wa Matarawe akiwa anaendesha piki piki alitumbukia mtoni na kufariki dunia papo hapo.
Hata hivyo Dkt.Nchimbi alilazimika kusimama na kushuka kwenye gari yake akiwa ameongozana na viongozi mbali mbali wa chama na Serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti ambapo Mbunge huyo aliwapa pole kwa ajali zinazotokea na kwa watu ambao wamepoteza ndugu zao alizungumza nao na kuwataka wawe na subira wakati ombi lao linashugulikiwa, majibu ambayo wanachi hao hawakulizika nayo
“Natoa pole sana kwa msiba na ajali ambazo zimetokea nimewasikia, na ninaahidi nitawajengea daraja hili ,kama nimeweza kujenga barabara hii kwa kiwango cha lami bila maandamano wala kufungiwa barabara nitashindwa daraja? hivi ni vitu vinavyozungumzika hili ni jambo dogo hivyo naomba twende kwenye mkutano wa hadhara na tutaongea vizuri zaidi , kwani ni kweli daraja ni finyu na linahitaji kufanyiwa maboresho zaidi, ‘alisema Dkt. N chimbi.
Dkt.Nchimbi akiwahutubia Wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya sekondari ya kutwa ya matarawe amesema,amesikitishwa na tukio hilo kwani tabia hiyo haipendezi ,haikubaliki na haina maadili na aina
tija kama wangekuwa na busara wangefika kwenye mkutano na kutoa kero zao badala ya kufanya fujo ambapo ameliagiza jeshi la polisi kuwasaka wahusika wa fujo hizo.
Amesema, ni kweli daraja hilo ni dogo ila siyo ustarabu kufunga barabara kwa masaa mawili kwani wamesababisha shughuli mbali mbali za maendeleo kusimama kutokana na barabara hiyo kufungwa na kwamba tayari ameshamuagiza Mhandisi wa halmashauri ya Manispaa hiyo kufanya tathmini ili kujua gharama zinazohitajika ili liweze kupanuliwa.
Mapema Diwani wa kata ya Matarawe James Makene aliungana na kundi kubwa la wananchi hao na alimweleza Nchimbi kuwa hiyo ni changamoto ambayo wakazi wa matarawe wamekuwa wakilia kila mara hivyo wanahitaji msaada wa kupanua daraja hilo ambalo limeonekana kuwa ni kero ya muda mrefu.
Kwa upande wake kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Deusdedit Msimeki ameeleza kuwa kufatia vurugu hizo tayari watu nane wanashikiliwa na wanaendelea kuhojiwa zaidi ili kuwabaini vinara wengine wa fujo waliowashawishi wananchi kufanya fujo hizo .
0 comments:
Post a Comment