MWANDISHI wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro amejeruhiwa vibaya baada ya kupig
wa risasi mbili jana alfajiri huko Kibamba, Dar es Salaam.
Katika tukio hilo linalodaiwa kufanywa na mzazi
mwenzake, Anthery Mushi ambaye alijiua baadaye, pia anadaiwa kumuua mama
yake Ufoo, Anastazia Saro.
Ufoo alipigwa risasi moja tumboni na kutokea
kwenye mbavu na nyingine ilipita kifuani hadi kwenye ziwa lake la kulia
na kutokea kwenye mkono wa kulia.
Baada ya tukio hilo, Ufoo alipelekwa katika
Hospitali ya Tumbi, Kibaha kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili ambako alifanyiwa upasuaji.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Kamishna Suleiman Kova alithibitisha kutokea kwa tukio hilo
lililosababisha vifo hivyo na kumjeruhi mwandishi huyo.
Kova alimtaja Mushi, ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Saro akidai kuhusika na tukio hilo.
“Mushi alimpiga risasi za kifuani mama yake Ufoo,
ambaye alifariki palepale. Pia alimpiga risasi mwandishi huyo na baadaye
alijiua kwa kujipiga risasi chini ya kidevu, risasi ambayo ilifumua kwa
kiasi kikubwa eneo la juu la kichwa chake.”
Kova aliwaambia waandishi wa habari waliokuwa katika Hospitali ya Muhimbili kuwa, vifo hivyo vimetokana na wivu wa mapenzi.
Mashuhuda wa tukio
Akizungumzia tukio hilo, mdogo wa mwandishi huyo,
Goodluck Saro alisema dada yake Ufoo na shemeji yake Mushi walikwenda
nyumbani kwa mama yao huko Kibamba saa 12.00 asubuhi na kwamba baada ya
kufika huko walikuwa na mazungumzo na mama yao ambayo hata hivyo,
hakuyafuatilia kwa kuwa alikuwa amelala.
Goodluck alisema, muda mfupi baadaye alisikia sauti ya mama yake, ikimwita; “Goodluck nakufa... Goodluck nakufa.”
Alisema alitoka chumbani na kwenda sebuleni ambako alimkuta Ufoo akiwa ameanguka chini huku akichuruzika damu. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment