BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NDEGE YA ABIRIA YAANGUKA NA ABIRIA WATATU WAMERIPOTIWA KUFARIKI DUNIA NCHINI NIGERIA.

NDEGE iliyokuwa imewabeba watu 27 imeanguka baada ya kukumbwa na hitilafu ya injini, muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndeg
e mjini Lagos.

Duru zinasema kuwa watu 5 wamefariki huku shughuli ya uokozi ikendelea na mtu mmoja akipata matibabu kwa majeraha mabaya aliyopata.

Ndege hiyo ya shirika la ndege la Associated Airlines, iliyokuwa na uwezo wa kubeba watu 30 ilianguka muda mfupi tu baada ya kuruka na kulipuka.

Aidha ilikua inaelekea mjini Akure Kusini Magharibi mwa nchi, kwa mujibu wa msemaji wa shirika la udhibiti wa safari za angani nchini humo.

Injini ya ndege ilikumbwa na hitilafu na kuisababisha ndege kuanguka na kuteketea.

Hata hivyo hakuna taarifa za kuthibitisha idadi ya watu waliofariki.
Ndega hiyo iliruka mwendo wa saa mbili unusu kutoka katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Murtala Mohammed
Maafisa walisema kuwa ndege hiyo ilianguka karibu na bomba la mafuta katika uwanja huo.

Haijulikani ikiwa mafuta hayo ndiyo yalisababisha ndege kulipuka.
Shahidi mmoja alimbia BBC kuwa alisikia mlipuko mkubwa uliofatiwa na moshi mkubwa ukifuka kutoka katika sehemu ya ajali hiyo.

Maafisa wa usalama waliharakisha kwenda katika eneo la ajali na kuanza kuwaokoa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo.BBC.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: