DAR ES SALAAM.
RAIS Jakaya Kikwete na viongozi wa vyama vya siasa vya CCM, Chadema, CUF, NCCR- Mageuzi, TLP na UDP wamekubaliana mambo mawili makubwa baada ya kuweka pembeni tofauti za kiitik
adi na kutanguliza masilahi ya taifa walipokutana jana Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete akisaliana na Freema Mbowe.
RAIS Jakaya Kikwete na viongozi wa vyama vya siasa vya CCM, Chadema, CUF, NCCR- Mageuzi, TLP na UDP wamekubaliana mambo mawili makubwa baada ya kuweka pembeni tofauti za kiitik
adi na kutanguliza masilahi ya taifa walipokutana jana Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete akisaliana na Freema Mbowe.
Mkutano huo uliitishwa na Rais Kikwete ili kuondoa
sintofahamu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko
ya Katiba uliopitishwa Septemba na Bunge lilipokutana mjini Dodoma.
JK akisalimiana na Mhe Tundu Lissu, kushoto ni Mhe James Mbatia.
JK akisalimiana na Mhe Tundu Lissu, kushoto ni Mhe James Mbatia.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano
Ikulu jana jioni ilisema katika mkutano huo ilikubaliwa kwamba vyama
vyote vya siasa nchini vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha
Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba viwasilishe
mapendekezo yao haraka serikalini ili ifatutwe namna ya kuyashirikisha
mapendekezo hayo katika marekebisho ya sheria hiyo.
Mhe John Mnyika akisalimiana na Rais Kikwete.
Mhe John Mnyika akisalimiana na Rais Kikwete.
Pia Rais na vyama hivyo walikubaliana kwamba vyama
vya siasa nchini, kama wadau muhimu katika mchakato wa Katiba Mpya,
viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na
maridhiano kwa lengo la kusukuma mbele mchakato huo kwa masilahi mapana
ya nchi yao na mustakabali wa taifa.
“Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimepewa
jukumu la kuratibu jambo hilo ikiwa ni pamoja na kuandaa mkutano wa
vyama hivyo na wadau wengine nchini,” iliongeza taarifa hiyo.
Viongozi wa vyama vyama vya siasa waliohudhuria
mkutano huo ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip
Mangula, Isaack Cheyo ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo
na Nancy Mrikaria ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa TLP, Augustine
Mrema. Cheyo na Mrema wako nje ya nchi.
Wengine ambao waliambatana na wenyeviti wao ni
Mohamed Mnyaa na Julius Mtatiro wa CUF, Tundu Lissu na John Mnyika wa
Chadema na Martin Mng’ongo wa NCCR-Mageuzi.
Vicheko Ikulu
Vicheko na bashasha vyatawala Ikulu
Ilikuwa fursa kwa Rais Kikwete kukutana na
viongozi hao baada ya kipindi cha miezi miwili cha kurushiana maneno
baina ya viongozi wa Bunge, Serikali, CCM waliokuwa wakivutana na
viongozi wa vyama vitatu vya Chadema, CUF na NCCR- Mageuzi.
Kama mtu yeyote angeulizwa kutabiri katika tukio
lililotokea jana lingetokea basi angekuwa na wakati mgumu kutokana na
ukali wa maneno na malumbano katika kipindi chote baada ya kumalizika
kwa mkutano wa Bunge wa Septemba. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment